Mkongwe katika gemu la muziki wa Bongo Fleva, Mwasiti Almas.
Alisema alijitunza sana akiwa shule ya msingi, akaendelea hivyo hadi alipomaliza masomo ya sekondari ndipo alipolegeza uzi na kujikuta ameanza kuvunja amri ya sita na kujua thamani ya mwanaume.
“Nilikuwa muoga sana, tangu shule ya msingi hadi sekondari sikuweza kabisa kufanya mambo ya kikubwa,” alisema.
“Nilikuwa muoga sana, tangu shule ya msingi hadi sekondari sikuweza kabisa kufanya mambo ya kikubwa,” alisema.
Akizungumza na Weekly Star Exclusive, Mwasiti alifungukia umri wake ambapo alikiri ‘eji’ imeenda lakini suala la kuolewa ataendelea kusubiri hadi muda muafaka utakapofika.
“Kuhusu umri kwa sasa nipo katikati ya 25 hadi 30, umri umeenda kidogo siyo mdogo mimi. Nitaolewa tu muda ukifika, sina haja ya kuharakisha,” alisema Mwasiti.
Mwasiti Almas akifanya mambo yake stejini.
Japo hakuanisha muda muafaka wa kuolewa, katika sentensi nyingine Mwasiti alisema anatamani sana kuzaa mwaka huu kwani amekuwa na hamu ya kuitwa mama.
Mwasiti ambaye juzikati ameachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Serebuka (audio na video), hivi karibuni alivuta mkoko mpya aina ya Rav 4 huku akiwa mbioni kukamilisha mjengo wake maeneo ya Mbezi ya Kimara, jijini Dar.
Post a Comment