Naibu Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Nchemba
akipokea Zawadi ya Ua wakati akipokewa na Wafanyakazi wa Wizara ya
Fedha jijini Dsm hii Leo,Tukio hili limefanyika Nje ya Wizara ya Fedha
ambapo mamia ya Wafanyakazi asubuhi ya Leo Tar.22/01/2014 walijitokeza
Kuwalaki Mawaziri wapya walioteuliwa na Rais Kikwete wiki iliyopita
ilikujaza nafasi za Mawaziri wanne Zilizokuwa Wazi kutokana na Kujiuzulu
pamoja na Kifo cha Waziri wa Fedha Marehemu Mgimwa.
Mh:Malima ambaye ni Naibu waziri wa Fedha akipokea Zawadi ya Ua wakati wa alipofika Rasmi Ofisini hii leo kwaajili ya Kuanza Majukumu yake baada ya Kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Naibu Waziri wa Fedha.
Mapokezi Yakiendelea Asubuhi ya Leo Nje ya Wizara ya Fedha.
Mapokezi
Yanaendelea,Watumishi wa Wizara ya Fedha walijitokeza Kwa wingi sana
kuwapokea Manaibu Waziri wapya wa Wizara hiyo.(Mh:Mwigulu Nchemba na
Mh:Adam Malima) Pembeni(Kushoto) ni Mkurugenzi wizarani hapo aliyeongoza
mapokezi hayo
Naibu Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Nchemba
akilakiwa na Maofisa wa Wizara ya Fedha mapema hii leo Asubuhi wakati
alipofika Ofisini hapo rasmi kuanza kazi.
Naibu
Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Nchemba akibadilishana Mawazo na Katibu Mkuu
wa Wizara ya Fedha wakati wa hafla ya Kuwapokea Mawaziri hao Wapya hii
leo zoezi lililofanyika Wizara ya Fedha na Kukamilika Jioni ya Leo.Picha Zote na HABARI KWANZA BLOG
Post a Comment