Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YAKAMILISHA ZOEZI LA KUWANOA WAKUFUNZI WA UTAFITI WA WATU WENYE UWEZO WA KUFANYA KAZI

 

PICHA NAMBA 1
Wakufunzi wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa sekta ya Elimu Wariambora Nkya (hayupo kwenye picha) aliyefunga mafunzo ya Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi mwaka 2014 kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendela
PICHA NAMBA 2
Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa sekta ya Elimu, Wariambora Nkya, (wapili kutoka kulia walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa mafunzo ya wakufunzi wa Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi mwaka 2014, mara baada ya kufunga mafunzi hayo, jana  kwenye ukumbi wa Edema, Mjini Morogoro  ( wapili kutoka kushoto) ni Mkurugenzi wa Sensa ya  watu na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephraim Kwesigabo.
( Picha zote na John Nditi).
……………………………………………………………
(Na Veronica kazimoto – Morogoro)
19 Januari, 2014.
Viongozi wote wa Serikali katika ngazi zote kwa ujumla wameombwa kutoa ushirikiano katika kuhamasisha na kuelimisha umma umuhimu wa kushirikiana na Wadadisi pamoja na Wasimamizi wa Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi unaotarajia kuanza rasmi mwezi Februari na kumalizika Disemba mwaka 2014.

Hayo yamesemwa jana na Katibu Tawala Msaidizi wa mkoa wa Morogoro Wariambora Nkya wakati akifunga Mafunzo ya Wakufunzi wa Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Edema mkoani Morogoro.
Nkya amefafanua kuwa ni muhimu viongozi wote wa Serikali kutoa ushirikiano kwa wadadisi na wasimamizi kwani utafiti huo ni muhimu katika kuboresha sera na program mbalimbali za kukuza ajira, kupanga na kufuatilia utekelezaji wa mipango ya maendeleo kama vile Malengo ya Milenia, Dira ya Maendeleo ya mwaka 2015 na Malengo ya MKUKUTA na MKUZA.
“Nitoe wito kwa viongozi wote wa Serikali kutoa ushirikiano kwa Wadadisi na Wasimamizi wa Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 ili waweze kutekeleza majukumu yao kama ilivyopangwa”, amesema Nkya.
Wakati huo huo Katibu Tawala Nkya amewaomba Wananchi kutoa ushirikiano wa kujibu maswali na kutoa taarifa sahihi wakati watafiti watakapopita katika makazi yao kukusanya taarifa za soko la ajira katika ngazi ya Kaya.
“Napenda kuwahakikishia Wananchi kwamba shughuli zao za kiuchumi na kijamii hazitasimamishwa na zoezi la Utafiti huu kwa kuwa Wadadisi watakusanya takwimu za Utafiti huu wakati shughuli zingine zikiedelea kama kawaida”,  amesisitiza Nkya.
Wariambora Nkya ameyasema hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendera na mafunzo hayo ya wiki mbili yaliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu yamemalizika ambapo jumla ya Wakufunzi 60 kutoka mikoa mbalimbali nchini walihudhulia mafunzo hayo.
Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Morogoro, Katibu tawala msaidizi  wa mwaka 2014 huu katika maeneo yatakayohusika. 
Ukosefu wa Ajira umekuwa ni changamoto kubwa kwa sasa duniani kote ambapo ripoti ya mwaka 2013 ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) kuhusu hali ya ajira duniani, inaonesha kuwa takribani  watu milioni 197 sawa na asilimia 5.9 ya nguvu kazi duniani hawana kazi.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Dkt. Milton Mahanga   wakati akifungua Mafunzo ya Wakufunzi wa Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Edema uliopo Morogoro mjini.
Dkt. Mahanga amesema kati ya watu 197 ambao hawana kazi vijana ni milioni 73.8 sawa asilimia 12.6 ambayo ni nguvukazi inayopaswa kutumika ipasavyo kwa kuwa kuna mahusiano makubwa kati ya ukuaji wa tija na matumizi ya nguvukazi.
Ameongeza kuwa, kutokana na changamoto hiyo ya ajira, ni muhimu kufanya Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya kazi ili kuisaidia Serikali kufuatilia mwenendo wa mabadiliko yanayotokea katika soko la ajira.
Mahanga amefafanua kuwa utafiti huu utasaidia pia kuboresha sera na program mbalimbali za kukuza ajira, kupanga na kufuatilia utekelezaji wa mipango ya maendeleo kama vile Malengo ya Milenia, Dira ya Maendeleo ya mwaka 2015 na Malengo ya MKUKUTA na MKUZA.
Kwa upande wa Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Ephraim Kwesigabo amesema lengo kuu la Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi ni kukusanya takwimu zinazohusu hali ya soko la ajira nchini.
Kwesigabo amesisitiza kuwa utafiti huo utawezesha  kupata viashiria vinavyohusu ajira na ukosefu wa ajira kwa makundi mbalimbali yaliyopo katika jamii na hivyo kuisaidia Serikali kuboresha sera ya kukuza ajira nchini.
Mafunzo hayo ya wiki mbili yameandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ambapo jumla ya Wakufunzi 60 kutoka mikoa mbalimbali nchini wanaendelea kupewa mafunzo juu ya Utafiti huo  wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi utakaoanza rasmi mwezi Februari hadi Disemba mwaka 2014.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top