Polisi
wa kupambana na ugaidi nchini Kenya wameanzisha uchunguzi kubaini
chanzo cha mlipuko mdogo uliotokea katika mkahawa mmoja katika uwanja wa
kimataifa wa ndege wa JKIA, Nairobi
Pia
wanachunguza ikiwa mwanamume raia wa Somalia aliyepatikana ameuawa
katika mtaa wa Shauri Moyo mjini Nairobi alihusika na mlipuko huo
Alhamisi usiku.
Mwili
wa mwanamume huyo mwenye umri wa makamo, ulipatikana katika kiti cha
nyuma cha gari iliyokuwa imefyatuliwa risasi nyingi karibu saa tano
asubuhi siku ya Alhamisi.
Ugunduzi huu ulijulikana saa moja baada ya mlipuko kuripotiwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta.
Gari hilo lilipatikana katika mtaa wa Shauri Moyo milango yote ikiwa imefunguliwa. Magurudumu ya gari hilo yalikuwa yamepasuka.
Walioshuhudia tukio hilo waliambia polisi kuwa wanaume wawili raia wa kisomalia, walishuka kutoka kwa gari hilo la kutoroka.
Polisi walipoangalia ndani ya gari walipata mwili wa mtu huyo ukiwa na damu .
Pia
walipata kikombe cha moja ya mikahawa iliyo katika uwanja huo , ishara
kuwa walikuwa wametembelea mkahawa huo ilio katika uwanja wa ndege.
Polisi waliweza kutegua bomu lililopatikana kwenye kiti cha nyuma cha gari hilo
Polisi pia wanachunguza picha za CCT za gari ambalo lilikaidi amri ya polisi kusimama likitoka katika uwanja huo wa ndege
Hata
hivyo awali, mkuu wa polisi David Kimaiyo alisema kuwa mlipuko
uliosikika katika uwanja huo ulisababishwa na Balbu ya ta iliyoanguka na
kusababisha moto.Chanzo BBC Swahili
Post a Comment