Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RAIS JK ALIPOMCHANA LIVE MBUNGE MWANASHERIA WA CHADEMA ASIYEJUA SHERIA LIVE!!

 

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi (kushoto) akizungumza na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa; kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Cuf, Prof Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, walipohudhuria hafla ya kukabidhi Rasimu ya pili ya Katiba Mpya iliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee Dar es Salaam, jana. Picha na Silvan Kiwale 
    ******
Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete amempiga kijembe Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu akisema amekuwa akiwachanganya wenzake katika masuala ya kisheria.
Rais Kikwete alisema hayo Dar es Salaam jana alipokuwa akizungumza katika hafla ya kupokea Rasimu ya Pili ya Katiba.
“Nawaona wanasiasa wenzangu wamehudhuria hafla hii muhimu, lakini pia namwona mwanasheria maarufu ambaye wakati mwingine amekuwa akizichanganya sheria zenyewe,” alisema Rais Kikwete huku akicheka.
Hali ilivyokuwa
Viongozi mbalimbali walifurika kwenye Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam wakati tume hiyo ilipokabidhi Rasimu ya Pili ya Katiba.
Kivutio cha watu wengi alikuwa Mwenyekiti wa Tume, Jaji Joseph Warioba ambaye alikuwa akishangiliwa karibu wajumbe wote wa tume hiyo.
Jaji Warioba aliwasili kwenye viwanja hivyo saa 6:45 akiwa amevalia suti ya rangi ya maziwa, huku akiongozana na Makamu wake Jaji Agustino Ramadhani.
Kabla ya kuketi, Jaji Warioba alisalimiana na viongozi mbalimbali wa Serikali waliokuwapo.
Baada ya Jaji Warioba kuwasili, viongozi wengine waliofuata ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais, Dk Mohamed Ghalib Bilal.
Miongoni mwa wanasiasa waliohudhuria hafla hiyo ni Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.
Mbali na viongozi hao, walikuwapo Mwanasheria Mkuu mstaafu wa Tanzania, Jaji Mark Bomani, George Kahama na Waziri Mkuu mstaafu, Cleopa Msuya.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top