Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Rais wa Zanzibar Dk Ali Shein amewaapisha Nd. Ahmed Kassim Haji kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais na Bibi Rukia Mohamed Issa kuwa Mjumbe wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma nchini.

 


Naibu Katibu Mkuu ,Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Ahmad Kassim Haji
Mjumbe Mpya wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma Bi. Rukia Mohamed Issa
----
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY  ZANZIBAR
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein jana amewaapisha Nd. Ahmed Kassim Haji kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais na Bibi Rukia Mohamed Issa kuwa Mjumbe wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma nchini.
Kuapishwa kwa watendaji hao kunafuatia uteuzi wao uliofanyika hivi karibuni ambapo Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi alimteua pia Dk. Mohamed Seif Khatib kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili Zanzibar.
 
Miongoni mwa viongozi waliohudhuria hafla hiyo ya kuapishwa ni pamoja na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mheshimiwa Omar Makungu, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Omar Saleh Kabi, Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Mheshimiwa Khatib Abdulrahman Khatib na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis. 
 
Postal Address: 2422 Tel.+255 776 613 015, Fax: 024 2231822 
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top