Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu
akizungumza wakati wa maadalizi ya ufungaji wa mafunzo ya vijana
wawakilishi wa vikundi kutoka mikoa mbalimbali kuhusu utengenezaji wa
matofali ya ya udongo yenye teknolojia ya Interlocking Blocks yaliyoanza
Januari 6 mpaka 17 mwaka huu ambayo yanatarajiwa kufungwa wiki ijayo na
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda,
Mkurugenzi huyo amesema Shirika la nyumba badala ya kwenda kutoa msaada
wa sabuni na vyakula katika vituo vya watoto yatima au kusaidia biskuti
limeamua kubadilisha maisha ya vijana wa Tanzania kwa kuwapa mafunzo na
kuwapatia mashine za kutengeneza matofali ya udongo ambayo wao NHC
watakuwa ndiyo wateja wakuu wa kununa matofali hayo, lakini pia shirika
hilo linatoa mashine za kufyatulia matofali zipatazo 640 katika wilaya
160 mikoa yote ya Tanzania bara na kiasi cha shilingi 500,000 kila mkoa
kama mtaji wa kununulia saruji kwa vikundi hivyo, Katikati ni Injinia
Kwanama Elias Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo kutoka Nation
Housing&Building Research Agency
(NHBRA) na kushoto ni Bw.Julius Njelwa kutoka VETA, mafunzo hayo
yameratibiwa kwa pamoja na (NHC), (VETA) na (NHBRA) kwa pamoja.(PICHA NA
KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM) Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu
akizungumza akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari leo.
Injinia Kwanama Elias Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo kutoka Nation Housing&Building Research Agency (NHBRA) akifafanua masuala ya kitaalamu kuhusu teknolojia hiyo ya matofali kwa waandishi wa habari.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo.
Baadhi
ya maofisa wa Shirika la Nyumba NHC wakiwa katika maadalizi hayo
kushoto ni Suzan Omary Meneja Mawasiliano NHC, Muungano Saguya Meneja
huduma kwa jamii NHC na Ephraim Kibonde mtangazaji wa Clouds Radio.
Post a Comment