Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

TASWIRA KAMPENI ZA UDIWANI TANDAHIMBA

 












Mh:Mwigulu Nchemba akiwasili eneo la Mkutano Kata ya Mkwiti Wilaya ya Tandahimba Mkoani Mtwara kwaajili ya Kufungua Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Udiwani,Licha ya Mvua Kubwa Kunyesha hadi mwisho wa Mkutano,Wananchi walikuwa radhi kunyeshewa lakini Wamsubiri Naibu Katibu Mkuu wa Chama Chao cha CCM ambaye kabla ya Kufika Mkutanoni alikuwa na Ziara ya Kufungua Matawi ya Chama,Kupokea Wananchama wapya waliojiunga na CCM Wilaya Ya Tandahimba na kutembelea Mashina ya Chama

 

Mh:Mwigulu Nchemba akitoa dakika Moja kwaajili ya Kumuombea Marehemu(aliyekuwa Diwani wa kata hii ya Mkwiti) ambayo hii loe inafanyiwa Uchaguzi Mdogo ilikuziba pengo lake Kiutendaji ndani ya chama na Serikali.


Mvua Kubwa ikiendelea Kunyesha,Naibu katibu Mkuu CCM Bara akiendelea kunadi Sera za CCM kwa Wakazi wa Kata ya Ikwiti kijiji cha Njia Panda,Mwigulu Nchemba amewaomba wananchi wa Ikwiti kumchagua Mgombea kwa CCM kwa sababu CCM imeshaanza kutekeleza Ilani yake ndani ya kata hiyo na Wilaya yote ya Tandahimba,Wananchi waliomba sana Kupewa Barabara ya Rami Mwaka 2010 wakati wa Kampeni,Rami imeshawekwa kadri ya Maombi yao,Pia soko la Korosho limeshaimarishwa.


 

Huyu alikuwa naye anawania Udiwani,Bahati mbaya kura zake hazikutosha wakati wa Mchujo lakini ameamua kumuunga mkono MwanaCCM mwenzake,Na sasa Ndiye meneja kampeni wa Mgombea wa CCM ndani ya Kata ya Mkwiti.

Ameloa chapachapa Naibu Katibu Mkuu kwa Mvua Kubwa iliyokuwa ikinyesha wakati wa Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni,Lakini Wananchi walikuwa wavumilivu vya Kutosha na hatimaye kushiriki Mkutano huo hadi dakika za Mwisho kwa Mapenzi yao Kwa Mgombea na Chama cha Mapinduzi

  

Naibu Katibu Mkuu CCM Bara akimnadi Mgombea wa Udiwani kata ya Mkwiti wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Nakatanda Arafa Twalib ambaye ni kada Mtiifu wa Chama Cha Mapindizi kuanzia Ujana wake,

Licha ya Mvua Kubwa iliyoanza Mapema tu kabla hata Mkutano kaunza,Wananchi walijitokeza kwa wingi Kwenye Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni za Udiwani Kata ya Mkwiti,Uchaguzi mdogo huu unaofanyika takribani kata 27 Nchi nzima kutokana na Madiwani waliochaguliwa Mwaka 2010 kwa sababu za Vifo na Kujuzulu nafasi hizo zimekuwa wazi kwa Muda mrefu na sasa Tume imeamua Uchaguzi Ufanyike tena.

Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa Mkwiti amewatolea Mfano mmoja Mwepesi sana "Ukiwa na Touchi yako unahitaji mwanga,Betri ya Kwanza Umeweka Vizuri(CCM-Rais),Betri ya Pili Umeweka Vizuri (CCM-Mbunge),Betri ya Mwisho unaweka Gunzi(Upinzani) Itawaka?,HIvyo basi ni Muda Muafaka Kwa WanaMkwiti Kuendelea kukiunga chama cha Mapinduzi kiendelea kuongoza ndani ya Kata yao ili maendeleo yatokanayo na Ilani ya CCM yafanyike kwa Ufanisi.

Kata ya Mkwiti imekuwa Ikiongozwa na CCM tangu k
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top