Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Ujumbe wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Oman Wawasili Zanzibar.






Balozi wa Tanzania Nchini  Oman Balozi Ali Ahmeid Saleh , akiongoza Ujumbe wa Wafanyabiashara wa Oman, wakiwa na Kiongozi wao Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara ya Oman (OCCI) wakiwasili katika bandari ya Zanzibar wakitokea Dar-es-Salaam, kwa ziara ya siku tatu kuonana na Wafanyabiashara wa Jumuiya ya Wafanyabiashara ya Zanzibar kuimarisha Umoja wao ulioundwa hivi karibuni baina ya Oman na Tanzania. 


Wafanyabiashara wa Oman wakipokelewa Balozi wa Mdogo wa Oman Zanzibar na Wenyeji wao Viongozi wa Jumuiya ya Wafayabiashara wa Zanzibar, wakiwasili kwa Boti ya Kampuni ya Azam Kilimanjari 4.

Viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Zanzibar wakiwapokea Wageni wao katika Bandari ya Zanzibar.


Balozi Mdogo wa Oman Zanzibar Balozi Khalid Khamis na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Oman Khalil Bin Abdallah Al Khonji wakiwasili katika bandari ya Zanzibar kwaziara ya siku tatu.. 



Balozi wa Oman Nchini Tanzania Balozi Ali Ahmeid Saleh, akiongoza Ujumbe wa Wafanyabiashara wa Oman Zanzibar.




Balozi wa Tanzania Nchini Oman Balozi Ali Ahmeid Saleh, akizungumza na Waandishi wa habari ujio wa Ujumbe wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Oman Zanzibar ili kukuza uhusiano wao wa makubaliano ya kuunda Jumuiya ya Pamoja ya Wafanyabiashara wa Oman na Tanzania.


Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Oman Bwa. Khalil Bin Abdullah Al Khonji, akizungumza na waandhishi wa habari baada ya kuwasili katika bandari ya Zanzibar kwa mazungumzo na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Zanzibar na kuimarisha uhusiano wa Kibiashara kati ya Zanzibar na Oman 


Wafanyabiashara wa Oman wakimalizia kujaza fomu za Uhamiaji baada ya kuwasili Zanzibar wakitokea Dar-es-Salaam, wakiwa Zanzibar watakuwa na Mkutano na Jumuiya ya Wafanyabiashara ya Zanzibar na Wafanyabiashara kuzungumzia kuimaridha Jumuiya ya pamoja ya Wafanyabiashara wa Oman na Tanzania  






Ujumbe wa Wafanyabiashara wa Oman wakitoka katika chumba cha VIP baada ya kumaliza taratibu zote za kiserekali za kuingia nchini. baada ya kuwasili na boti ya kampuni ya Azam Marine ya Kilimanjaro 4.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top