Mwenyekiti wa UVCCM Taifa -Sadifa Juma Khamis.
Mwenyekiti
wa jumuiya ya umoja wa vijana CCM (UVCCM) wilaya ya Singida
mjini,Ibrahimu Ramadhani akizumgumza kwenye mkutano wa wanachama wa CCM
wa tawi la chuo cha uhasibu cha tawi la mkoa wa Singida.
Mwenyekiti wa jumuiya ya
umoja wa vijana CCM (UVCCM) wilaya ya Singida,Ibrahimu Ramadhani (wa
kwanza kushoto) akifurahia jambo na mjumbe wa halmashauri kuu (NEC) CCM
taifa kupitia UVCCM,Jonathan Nkya ambaye alikuwa mgeni rasmi katika
mkutano wa wanachama wa CCM chuo cha uhasibu tawi la mkoa wa Singida.
Baadhi ya wananchama wa
CCM chuo cha uhasibu tawi la mkoa wa Singida wakimsikiliza kwa makini
mjumbe wa halmashauri kuu (NEC) CCM taifa, Jonathani Nkya (hayupo kwenye
picha).Picha na Nathaniel Limu.
Na Nathaniel Limu, Singida
MJUMBE
wa Halmashauri kuu (NEC) CCM taifa kupitia Jumuiya ya Umoja wa Vijana
(UVCCM), Jonathan Nkya amevuna wanachama wapya 248 waliojiunga na Chama
Cha Mapinduzi.
Wanachama hao wapya, ni wanafunzi wa chuo cha Uhasibu tawi la mkoa wa Singida.
Akizungumza
hivi karibuni na wanachama hao wapya wa CCM, Nkya aliwatahadharisha na
wanasiasa ambao malengo yao ni kupandikiza sera ambazo zimekuwa chachu
na chanzo cha migogoro katika vyuo mbalimbali.
Aliwataka
wawe makini na wanasiasa hao wenye lengo la kujitafutia umaarufu
binafsi kwa kupandikiza sera zisizokuwa na tija zaidi ya kupandikiza
chuki na migogoro isiyoisha..
Katika
hatua nyingine Mnec huyo, amewataka wanafunzi wa vyuo vya uhasibu
watakaobahatika kuajiriwa na halmashauri za wilaya, manispaa na majiji,
kutumia taaluma ya vizuri kudhibiti wizi wa fedha na umma, ambao
unapigiwa kelele kila kona ya nchi.
Amesema
fedha za umma zinazopelekwa kwenye halmashauri kwa ajili ya maendeleo
ya wananchi ni nyingi mno, lakini kiwango kikubwa cha fedha hizo,
zinaishia kwenye mkono wa watumishi wasio waaminifu.
“Ninyi
mkimaliza masomo yenu, muwe wazalendo wa kweli wa nchi yenu, katika
kudhitibiti na kuhakikisha fedha za umma zinatumika kwa malengo
yanayokusudiwa tu, na si vinginevyo” amesema Nkya ambaye ni mhadhiri wa
chuo kikuu cha Mzumbe.
Awali
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Singida mjini, Ibrahimu Ramadhani,
aliwapongeza wanachama hao wapya kwa uamuzi wao wa busara wa kujiunga na
chama chenye sera zinazotekelezeka.
Aidha
amewahimiza kusoma kwa bidii na kwa malengo, kujiepusha kabisa na
vitendo vitakavyochangia kufanya vibaya kwenye mitihani yao.
Post a Comment