Baraza
kuu la waislamu Tanzania (BAKWATA) limekemea vitendo vinavyofanywa na
baadhi ya waumini wa dini hiyo ya kuvamia na kupora misikitini na
kusbabisha uvunjifu wa amani,akitoa salam za baraza hilo kwenye Baraza
la Maulid lililofanyika mjini Kigoma, Naibu Katibu
Mkuu wa BAKWATA, Sheikh Mohamed Khamisi amesema kuwa vitendo vya uporoaji wa madaraka kwenye misikiti na umwagaji damu ni kinyume na muenendo na mafundisho ya dini.
Mkuu wa BAKWATA, Sheikh Mohamed Khamisi amesema kuwa vitendo vya uporoaji wa madaraka kwenye misikiti na umwagaji damu ni kinyume na muenendo na mafundisho ya dini.
Kutokana na hilo amesema kuwa baraza hilo halina budi kukemea kwa
nguvu vitendo hivyo na kuwaonya waislam kuacha mara moja kwani vimekuwa
vikiipaka matone na kuunajisi uislam.
Akizungumzia jambo hilo kwa niaba ya serikali Mkuu wa mkoa Kigoma,
Issa Machibya amesema kuwa serikali haitasita kuwachukulia hatua kali
watu wote watakaobainika kuhusika katika vitendo vya uporaji madaraka na
kufanya mapinduzi kwenye
misikiti na kupelekea uvunjifu wa amani na umwagaji damu.
misikiti na kupelekea uvunjifu wa amani na umwagaji damu.
Post a Comment