Kamanda wa Polisi, mkoa wa Singida, SACP Geofrey Kamwela akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake.
*******
Na Nathaniel Limu, Singida
WATU
wasiofahamika idadi na makazi yao,wamevamia nyumba ya Daudi Karata (71)
mkulima na mkazi wa kijiji cha Nguamghanga tarafa ya Mgori wilaya ya
Singida mkoa wa Singida,na kunyang’anya bunduki aina ya shot gun na
risasi zake nne.
Kabla
na kufanya unyang’anyi huo,kundi hilo la watu wasiofahamika,lilimkata
kata mapanga mzee Karata sehemu mbalimbali za mwili kwa lengo la
kufanikisha azma yao kwa urahisi zaidi.
Kamanda
wa Polisi, mkoa wa Singida, SACP Geofrey Kamwela amesema tukio hilo
limetokea januari 21 mwaka huu saa tano asubuhi huko katika kijiji cha
Nduamghanga tarafa ya Mgori.
Amesema
mzee huyo Karata,alipatiwa matibabu katika kituo kidogo cha kutolea
huduma za afya kilichoandaliwa kwa muda kijijini hapo.
“Jeshi
la polisi linaendelea na msako mkali ili kuwakamata watu hao na
kuwafikisha mahakamani.Pia linatoa wito kwa raia wema kutoa taarifa
pindi wapatapo taarifa zo zote juu ya tukio hilo”,amesema kamanda
Kamwela.
Habari
kutoka kijiji hicho cha Nduamghanga,zinadai kwamba baada ya mzee Karata
kunyang’anywa bunduki yake shot gun,saa mbili baadaye,kundi la watu
zaidi ya 300 wakazi wa kijiji cha Handa wilaya ya Nchemba mkoa wa
Dodoma,walivamia kijiji hicho huku wakiwa wamebeba mapanga,rungu,pinde
na bunduki moja.
Kundi hilo linadaiwa kumuuawa mhudumu wa wanyamapori wa kijiji hicho,Athumani Jumanne Mkatapori kwa kumkata kata kwa mapanga.
Kundi
hilo linadaiwa lilikuwa linataka kuwakomboa ng’ombe wao 180
waliokamatwa kwa kuchungia ndani ya hifadhi ya akiba ya msitu wa Mgori.
Hata
hivyo,kundi hilo,halikuweza kuwapata ng’ombe wao na badala yake
likaishia kunyang’anya ng’ombe 68,mbuzi 101,kondoo sita na punda watatu
mali ya Abrahamani Mohammed (60) na kutokomea nao kusikojulikana.
Post a Comment