Waziri
Mkuu Mhe. Mizonge Pinda akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Nyumba la Taifa Nehemia Mchechu mara baada ya kuwasili katika Ofisi za
Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi ambapo
alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya ufungaji wa mafunzo kwa Vijana
waliowezesha kupata taaluma ya utengenezaji wa matofali kwa teknolojia
ya kisasa. leo jijini Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungana wa Tanzania Mizengo Pinda akisalimiana na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sihaba
Nkinga wakati alipo wasili katika hafla ya ufungaji wa mafunzo kwa
vijana kuhusu utengenezaji wa matofali leo jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara
akimkaribisha Waziri Mkuu ali aweze kuzungumza na Vijana wahitimu wa
mafunzo ya ujenzi wa matofali kwa teknolojia ya kisasa na gharama nafuu
leo jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayoyamenedeshwa na Wakala wa Utafiti
wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi(NHBRA), kwa kushirikiana na Shirika
la Nyumba la Taifa (NHC) na na kushirikisha idadi ya washiriki 50 kutoka
sehemu mbalimbali hapa nchini.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungana wa Tanzania Mizengo Pinda akihutubia
wahitimu pamoja na wageni waalikwa katika hafla ya ufungaji wa mafunzo
kwa vijana kuhusu utengenezaji wa matofali kwa kutumia teknolojia ya
kisasa na kwa gharama nafuu iliyofanyika katika ofisi za Wakala wa Taifa
wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) leo jijini Dar es
Salaam.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungana wa Tanzania Mizengo Pinda akiangalia baadhi
ya Matofali ambayo tayari yamekwisha tengeznezwa kwakutumia teknolojia
waliyofundishwa wahitimu hao leo jijini Dar es Salaam kushoto ni Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara.
Baadhi
ya wahitimu wa mafunzo ya Ufundi wa utengenezaji Natofali kwakutumia
teknolojia ya kisasa na kwa gharama nafuu wakimsikiliza Waziri
Mkuu(hayupo pichana) wakati akiwahutubia kwenye hafla ya kufunga mafunzo
yao na kuwakabidhi vyeti.
Picha zote na Frank Shija – Wizara ya Habari
Post a Comment