Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Mohammed Jiddawi na Dk. Peter McGovern wakitia
saini makubaliano ya kuanzisha huduma za Aya ya magonjwa ya akili
katika Hospitali ya Makunduchi. Katikati ni Naibu Waziri wa Afya Dk.
Sira Ubwa Mamboya akishuhudia utiaji saini katika sherehe zilizofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
Dk. Ingvar Bjelland kutoka Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukeland nchini
Norway na Daktari bingwa wa magonjwa ya akili wa Hospitali ya Kidongo
chekundu wakitia saini makubaliano ya kuanzishwa huduma za magonjwa ya
Afya ya akili katika Hospitali ya Makunduchi Kusini Unguja.
Dk.
Ingvar Bjelland kutoka Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukeland nchini
Norway akitoa maelezo jinsi Hospitali hiyo itakavyotoa huduma ya
magonjwa ya Afya ya akili Zanzibar katika sherehe za kutiliana saini
zilizofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar. Picha na Makame
Mshenga-Maelezo Zanzibar.
====== ====== ==========
RAMADHANI ALI/MAELEZO ZANZIBAR .
Wizara
ya Afya ya Zanzibar imetiliana saini mkataba wa makubaliano wa
kuanzishwa kwa majaribio kutolewa huduma za maradhi ya afya ya akili
katika Hospitali ya Makunduchi iliyoko Mkoa wa kusini Unguja.
Uwamuzi
wa kuifanya Hospitali ya Makunduchi kuanzisha huduma hiyo inatokana
na mapendekezo ya Wizara ya Afya ya mwaka 2008 na taarifa ya Afya ya
akili Zanzibar ya Jumuia ya Ulaya.
Wadau
watatu wanashirikiana katika mpango huo ambao ni Hospitali ya Chuo
Kikuu cha Haukeland cha Norway, Hospitali ya Afya ya akili ya
Kidongochekundu na Mradi wa kuimarisha Afya Zanzibar.
Katika
sherehe za utiaji saini zilizofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja, Wizara
iliwakilishwa na Katibu Mkuu Dk. Mohammed Jiddawi, Chuo Kikuu cha
Haukeland kiliwakilishwa na Dk. Ingavr Bjelland, Dk. Peter McGovern
alitia saini kwa upande wa Mradi wa kuimarisha Afya kijiji cha
Makunduchi na Dk. Khamis Othman alitia saini kwa upande Hospitali ya
Kidongo Chekundu.
Wadau
hao watatu watashirikiana katika kuimarisha kujenga uwezo huduma za
maradhi ya Afya ya akili kwa visiwa vya Unguja na Pemba, kuanzisha
mtaala wa kufundisha masomo ya afya ya akili wafanyakazi wa Hospitali ya
Makunduchi kwa mujibu wa Shirika la Afya duniani (WHO) na kuunga
mkono maendeleo ya mafunzo yanayotolewa kwa wauguzi wa Hospitali ya
Makunduchi na Hospitali ya Kidongo chekundu.
Katika
hatua za awali zitakazoanzia mwaka huu, kliniki ya afya ya magonjwa ya
akili ya Hospitali ya Mkunduchi itasimamiwa kwa kiasi kikubwa na
Hospitali ya Kidongo chekundu na mafunzo yatatolewa katika mwaka wa
kwanza wa kuanzishwa huduma katika Hospitali hiyo.
Hatua ya
pili ya mpango huo itakayoanza mwezi Januari mwakani ambapo kliniki
hiyo itakuwa imeimarika na Hospitali mama ya Kidongo chekundu kuridhika
na hatua iliyofikia, Hospitali hiyo itaruhusiwa kujiendesha yenyewe
katika masuala mbali mbali ya uongozi na tiba. Kwa mujibu wa makubaliano
hayo Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukeland itasimamia na kuimarisha
mitaala ya elimu ya magonjwa ya Afya ya akili kwa wafanyakazi wa
Hospitali ya Makunduchi ikiwemo kusimamia mafunzo hayo.
Wadau
wote kwa pamoja wamekubaliana kuendeleza na kuimarisha huduma
za magonjwa ya afya ya akili katika kliniki ya Makunduchi kwa mujibu wa
misingi ya Shirika la Afya Duniani. Hospitali ya Makunduchi itakuwa
ni ya pili kutoa huduma za magonjwa ya Afya ya akili kwa kisiwa cha
Unguja na kwa Kisiwa cha Pemba huduma hiyo bado inaendelea kutolewa
katika Hospitali ya Chake Chake tu.
Post a Comment