Baada
ya kusoma na kuangalia baadhi ya blogs zinazoonesha udhalilishaji wa
Dada zetu Hapa Tanzania, nikaona bora na mimi nitoe somo kidogo,
Somo
langu si kubwa sana lakini ni la Muhimu sana kwa wasichana wanao
jiheshimu na kutaka kulitunza Hekalu takatifu, (mwili ulio umbwa na
kubarikiwa na Mungu mwenyewe.
Chumbani
ni sehemu ya Siri, ambayo inamfanya mtu ajitawale na kufanya matendo
ambayo hayawezi kufanywa mbele ya hadhara, ikiwemo na kuvua nguo,
kujaribisha nguo, kulala ukiwa mtupu kwa kujiamini, na kufanya lolote
ambalo mbele za watu utaona Aibu.
Lakini
sasa nimeona mambo ya chumbani yanafanyika hadharani kwa kutupa picha
za video na mnato kwenye mitandao sijajua kwa maana gani ila mambo hayo
yanawaweka watu Fulani Fulani kwenye utata sana hasa Dada zetu.
Picha za utupu.
Mimi
naamini kuwa Picha hizi hupigwa kwa usiri mkubwa lakini utunzaji wake
si wa Siri tena. Laptops na simu zetu za mikononi, ndio zinazo waumbua
wengi sana, hasa zinapo haribika, na kuhitaji kupeleka kwa mtaalamu
atengeneze.
Kuna
Msichana mmoja alijikuta anatembeza penzi lake kwa wanaume karibu sita,
baadaye akagundua kuwa anajidhalilisha na mwisho kupatwa na ugonjwa wa
zinaa, ambao kwa sasa amepona lakini hiyo life experience imemfanya
asiwe na furaha ya maisha kwa sasa.
Sababu
kubwa alipiga picha wakiwa watupu na mpenzi wake, na mwisho wasiku zile
picha zika vuja na kupelekwa mtandaoni, na zingine kusambaa kwenye simu
za watu.
Ushauri
wangu. Wasichana msikubali kupiga picha za utupu, kwasababu
zinaudhalilisha uanamke wako na kukuvunjia heshima maisha yako yote.
Kwani kitu kikisha ingia mtandaoni, hakitoki. Labda admin aamue kukitoa.
Na Watu wanatabia ya kushare, hata mmoja akitoa, wengine wanakuwa
wamesha download, na kuweka kwenye mitandao yao, hicho ndicho kibaya
zaidi.
Kuna
msanii mmoja anatafuta umaarufu kwa kupiga picha za mamna hiyo na
kuziweka mtandaoni, yeye amependa je Hao wasichana wanapenda?
Mwisho wa siku tujaribu kukumbuka tuliko tokea
Post a Comment