Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

ZAIDI YA KAYA 130 ZIMEKOSA MAKAZI YA KUDUMU MTWARA





Zaidi ya Kaya 130 zilizopo katika kata ya Nanyamba, wilaya ya Mtwara, zimekosa makazi ya kudumu kufuatia nyumba zao kubomolewa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo, iliyonyesha usikuwa juzi kuamkia jana

Akiongelea hilo, Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Wilman Ndile(Pichani juu allisema mvua kubwa ya zaidi ya mililita 200 ilinyesha na kusababisha maafa makubwa kwa wananchi kukosa makazi, vyakula na malazi hivyo kuhitajika kwa msaada wa haraka kuwanusuru na hali ngumu ya maisha.

“Nyumba 37 hizi zimebomoka kabisa, ni kifusi kabisa, nyumba nyingi zimeezuliwa paa, zingine zimetitia na kutanda nyufa…hawa wote tumewahamisha kwenye nyumba hizo na kwa sasa wamehifadhiwa kwa majirani zao, wakati tunaangalia utaratibu wa kuwasaidia” alisema Ndile 


Alibainisha kuwa ofisi yake imeomba chakula cha msaada kutoka ofisi ya waziri mkuu kitengo cha maafa zaidi ya tani 250 za mahindi kwa ajili ya wahathirika wa tukio hilo.
 

“Wapo watakaopatiwa bure mahindi hayo na wale watakaouziwa kwa bei ya sh.50 kwa kilo kutokana na uwezo wa waathirika…mahindi haya yatawasili Jumatatu na yataanza kugaiwa siku hiyohiyo” alisema DC Ndile
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top