Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

BUNGE LA KATIBA, NI VITUKO VITUPU

 

Bunge la Katiba vituko tupuMWENYEKITI wa CHADEMA, Freeman Mbowe ambaye pia ni mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, jana alinusuru mchakato wa uchaguzi wa mwenyekiti wa muda baada ya kuibuka vituko.
Mbowe katika ushauri wake alitaka mchakato huo uanze upya kwa karatasi za kura kugawiwa kwa utaratibu makini ili kila mmoja apige kura huku milango ikiwa imefungwa.
Ushauri wake ulikubaliwa na mwenyekiti wa kikao hicho ambapo mchakato ulifanyika upya kwa usimamizi mkali wa polisi, huku Bunge likiahirishwa kwa robo saa kutoa fursa ya kura kuhesabiwa.
Awali vituko kejeli na malumbano vilitawala zaidi uchaguzi huo wa Bunge lililoanza vikao vyake jana mkoani hapa.
Dalili za kuvurugika kwa uchaguzi huo zilianza kuonekana mapema kutokana na idadi kubwa ya wajumbe kusimama na kuwasha vipaza sauti bila kufuata taratibu walizoambiwa mapema.

Kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya katiba, mwenyekiti huyo wa muda atakuwa na jukumu la kuandaa na kupitisha kanuni za Bunge hilo zitakazotumika katika mijadala mbalimbali.

TANZANIA DAIMA
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top