Ndugu Mahmoud Thabiti Kombo
Mahmoud Thabit Kombo mgombea kwenye uchaguzi mdogo kwa tiketi ya CCM ameibuka mshindi kwa asilimia 76.5 kwenye uchaguzi mdogo wa uwakilishi uliofanyika leo Jimbo la Kiembe Samaki.
Matokeo kamili ya Uchaguzi Mdogo wa Uwakilishi Jimbo la Kiembe Samaki ni kama ifuatavyo
CCM 1856 sawa na aslimia 76.5
CUF 445 sawa na asilimi 18.3
ADC 84 sawa na asilimi 3.5
CHADEMA 34 sawa na asilimia1.4
Tadea 6 sawa na aslimia 02
SAU 1 sawa na asilimia 00
Mahmoud Thabit Kombo mgombea kwenye uchaguzi mdogo kwa tiketi ya CCM ameibuka mshindi kwa asilimia 76.5 kwenye uchaguzi mdogo wa uwakilishi uliofanyika leo Jimbo la Kiembe Samaki.
Matokeo kamili ya Uchaguzi Mdogo wa Uwakilishi Jimbo la Kiembe Samaki ni kama ifuatavyo
CCM 1856 sawa na aslimia 76.5
CUF 445 sawa na asilimi 18.3
ADC 84 sawa na asilimi 3.5
CHADEMA 34 sawa na asilimia1.4
Tadea 6 sawa na aslimia 02
SAU 1 sawa na asilimia 00
Mgombea
wa Chama cha ADC Mhe. Amani Ismail Rashid akisaini fomu ya Matekeo ya
Uchaguzi Mdogo wa Jimbola Kiembesamaki Zanzibar baada ya kutangazwa
mshindi.
Mshindi
wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar Mhe. Mahmuod Thabit
Kombo, akizungumza na Waandishi wa habari na kutowa shukrani kwa wapinga
kura wake na WanaCCM waliomuunga mkono katika safari ya Kampeni na
kuahidi kutimiza ahadi zote alizoahidi kwa Wananchi wa Jimbola
Kiembesamaki na kuondo kero zote na kuwaletea maendeleo katika jimbo
lao.
Mgombea
wa Chama cha SAU Ramadhani Simai akizungumza na Waandishi wa habari na
kumpongeza Mgombea wa CCM Mhe. Mahmuod Thabit Kombo kwa ushindi wake
aliopata katika zoezi hilo la uchaguzi mdogo wa jimbo la Kiembesamaki na
kuyapokea matokea hayo kwa mikonomiwili.
Mgombea
wa Chama cha TADEA Mhe. Ali Mohammed Ali ameridhika na matokea hayo
yaUchaguzi na ameridhika na kukiri hakuna Mamluki waliopita kupiga kura
katika vituo hivyo na kusema waliopiga kura ni Wananchi wa Kiembesamaki
tafauti na vyama vingine wanaolalamikia matokea hayo kuwa sio ya haki.
Uchaguzi ulikuwa ni wa Huru na Haki.
Na kusema chama chake kinajipanga Upya kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Kiongozi
wa Chama cha Siasa Zanzibar Mhe. Mshenga akielezea hali ya Uchaguzi
Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki uliokuwa ni wa Huru na Haki, hakuna
mizengo iliofanyika katika Uchaguzi huo, Amesema amatembelea vituo vyote
na kuridhika na hali ya upigaji kura kwa Wananchi wa jimbo hilo,
Uchaguzi umekwenda kwa Amani bila ya vurugu hali hii ndiyo Ustaarabu wa
Zanzibar kuwa na utulivu na amani wakati chaguzi.
Viongozi
wa Chama cha ADC, wakibadilishana mawazo baada ya kutangazwa mshindi wa
kiti cha Uwakilishi jimbo la Kiembesamaki wakijipongeza kwa ushindi
walioupata wa kura 84 kwa mara ya kwanza kushiriki uchaguzi kwa Zanzibar
na kujipa moyo watafanikiwa katika Chaguzin Kuu mwaka 2015. kutokana na
matokeo hayo yanatia moyo kwa Chama chao.


Post a Comment