MSHAMBULIAJI
Robert Lewandowski amejikuta katika wakati mgumu mjini Dortmund tangu
atangaze kuhamia kwa wapinzani Bayern Munich mwishoni mwa msimu- na sasa
watu wameamua kumfanyizia kweli.
Mpachika
mabao huyo wa Poland aliamka jana asubuhi na kukuta gari yake aina ya
Porsche Cayenne GTS imeng'olewa matairi yote manne nyumbani kwake eneo
la Schuren, Dortmund.
Gharama
za kununua matairi mengine ya kuweka kwenye gari ya Lewandowski in
Pauni 2,000, lakini wezi hao pia wameiharibu gari hiyo chini ya bodi na
kuvuruga mfumo wa breko, maana yake itamgharimu zaidi kufanya
marekebisho. Bei ya kununua gari mpya kama hilo ni kiasi cha Pauni
70,000.
Wamekomba: Wezi wameiba tairi zote nne za gari ya Robert Lewandowski aina ya Porsche Cayenne GTS usiku wa Jumapili
Marekebisho:
Tairi zote nne mpya za gari hii yenye thamani ya Pauni 70,000 ni Pauni
2,000, lakini wezi hao wameharibu zaidi chini ya gari ikiwemo mfumo wa
breki, hivyo zitahitajika gharama zaidi za matengenezo
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 25 atakayehamia Allianz Arena baada ya
kukamilisha msimu huu akiwa na Dortmund, alifunga mabao mawili katika
ushindi wa 5-1 dhidi ya Werder Bremen usiku wa Ijumaa na kufikisha mabao
18 msimu huu katika mechi 29.
Hii
si mara ya kwanza kwa nyumba ya Lewandowki kuingiliwa na wezi - nyumba
yake ya awali iliingiliwa kabla ya Krisimasi mwaka 2012.
Understandably, Lewandowski has not had a smooth time since announcing his departure on a free transfer.
Mkali
wa mabao: Lewandowski akishangilia baada ya kufunga moja ya mabao yake
mawili katika ushindi wa Dortmund wa 5-1 dhidi ya Werder Bremen Ijumaa
usiku
Post a Comment