*40 KUNG’AMUA VIPAJI UBORESHAJI TAIFA STARS
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeteua kikosi cha makocha 40 kutoka
sehemu mbalimbali, Tanzania Bara na Zanzibar ili kung’amua vipaji katika
mpango wa kuboresha timu ya Taifa (Taifa Stars).
Makocha
hao ambao watafanya kazi hiyo katika michuano maalumu ya mikoa
wanatakiwa kuripoti katika ofisi za TFF siku ya Jumamosi (Februari 8
mwaka huu) saa 4 asubuhi kwa ajili ya kupewa maelekezo zaidi.
Walioteuliwa
ni Abdallah Hussein (Kilimanjaro), Abdul Mingange (Dar es Salaam), Ali
Bushiri (Zanzibar), Ali Mayay (Dar es Salaam), Ally Mtumwa (Arusha),
Ayoub Selemani (Zanzibar), Boniface Pawasa (Dar es Salaam), Dan Korosso
(Mbeya), Dk. Mshindo Msolla (Dar es Salaam) na Edward Hiza (Morogoro).
Elly
Mzozo (Dar es Salaam), Fred Minziro (Dar es Salaam), George Komba
(Dodoma), Hafidh Badru (Zanzibar), Hamimu Mawazo (Mtwara), Idd Simba
(Mwanza), Jabir Seleman (Zanzibar), John Tegete (Mwanza), Juma Mgunda
(Tanga) na Kanali mstaafu Idd Kipingu (Dar es Salaam).
Kenny
Mwaisabula (Dar es Salaam), Khalid Abeid (Dar es Salaam), Madaraka
Bendera (Arusha), Madaraka Selemani (Dar es Salaam), Mbarouk Nyenga
(Pwani), Mohamed Mwameja (Dar es Salaam), Musa Kissoki (Dar es Salaam),
Nicholas Mihayo (Dar es Salaam), Patrick Rweyemamu (Dar es Salaam) na
Peter Magomba (Singida).
Peter
Mhina (Songea), Salvatory Edward (Dar es Salaam), Salum Mayanga
(Morogoro), Sebastian Nkoma (Dar es Salaam), Sekilojo Chambua (Dar es
Salaam), Shaban Ramadhan (Zanzibar), Steven Nemes (Dar es Salaam),
Sunday Manara (Dar es Salaam), Tiborowa Jonas (Dar es Salaam), Yusuf
Macho (Dar es Salaam), Zamoyoni Mogela (Dar es Salaam),
*QUALITY GROUP YAIPIGA JEKI TFF
Kampuni
ya Quality Group Limited imetoa sh. milioni 10 kwa Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) kwa ajili ya kuunga mkono mikakati ya shirikisho
la katika kuendeleza mpira wa miguu nchini.
Mchango
huo wa Quality Group utatumika katika programu mbalimbali za kuendeleza
mpira wa miguu nchini ambapo tunaishukuru kampuni hiyo kwa kuunga mkono
mikakati yetu.



Post a Comment