Wananchi wenye hasira kali wameteketeza kwa moto zaidi ya nyumba
ishirini na kuvunja nyingine katika kijiji cha Kilombero mkoani Geita
kutokana na mauaji ya watu watano yaliyotekelezwa kwa nyakati tofauti
kwa kukatwa mapanga.
Tukio la Februari 6 la mwanamke Felista Mathias kuuawa kwa mapanga limewachochea zaidi wananchi hao kuvamia nyumba za wanaodaiwa kuhusika februari 17 wakati ukoo ya Kisumo ukitajwa kuhusika na mauaji yanayotokea kijijini humo ambapo mmoja wao Elias Kisumo amekamatwa.
Kumekuwa na matukio ya mauaji ya mapanga kwa wazee katika kijiji hiki, na matukio hayo yanahusisha ushirikina, uvamizi wa mifugo katika mashamba ya watu na hata visasi.
kuuwawa kwa mwanamke FELISTA MATHIAS mwenye umri wa miaka 55 sababu kubwa ni Ngombe wake kula mahindi shambani kwa Elias Kisumo na kudai alipwe fidia na baada ya kulipwa usiku vijana watano walimvamia mwanamke huyo na kumuua kwa mapanga.
Kura zimepigwa na wanakijiji za kuwabaini wanaohusika na mauaji lakini Watendaji wa vijiji wameonekana kufumbia macho matukio haya hivyo siku kumi zimetolewa kuhakikisha wahusika wanakamatwa.
Wanakijiji wengi wamekimbia akiwemo mtuhumiwa Katibu wa sungusungu korogwe Kisumo anayetuhumiwa kwa mauaji, Katika mkoa wa Geita wilaya ya Bukombe na Geita zinaongoza kwa matukio ya mauaji ya wazee.

Post a Comment