Wito
umetolewa kwa wadau mbalimbali kuona ni namna gani wanaweza kupunguza kasi ya
kuenea kwa maambukizi ya UKIMWI katika mkoa wa Iringa.
Hayo
yamesemwa mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa wa Iringa Dokta Christina
Ishengoma alipokuwa akifungua semina ya usambazaji wa matokeo ya tafiti za
Kitaifa na mpango wa mikakati kwenye mikoa ya Nyanda za juu kusini Iringa, Njombe na Mbeya katika ukumbi
wa VETA mkoani Iringa.
Semina
hiyo ambayo imehudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka Shirika la umoja wa mataifa
linaloshughulikia watoto (UNICEF), Usaids Tanzania, Tume ya kudhibiti UKIMWI
(TACAIDS), Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Wizara ya maendeleo ya jamii
jinsia na watoto, Wataalamu toka Halmashauri za wilaya, Asasi zisizo za
kiserikali za vijana, Mtandao wa watu wanaoishi na virus vya ukimwi pamoja na
wawekezaji inatarajia kufanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 11 mpaka tarehe 13
februari mwaka huu.
Dokta
Ishengoma alisema kasi ya maambukizi imeongezeka kupita wastani wa Taifa wa
asilimia 5.1 hasa kwenye mikoa iliyokuwa na kiwango cha chini kama Iringa
kutoka asilimia 3 mwaka 2008 imeongezeka mpaka asilimia 9.1 mwaka 2012 hivyo
kwa matokeo hayo yanatahadharisha kuwa ni lazima kuwe na mbinu mbadala wa
kukabiliana na ongezeko la maambukizi ya UKIMWI.
Pia
amesema mkoa wa Iringa umeona kuna umuhimu wa kuongeza jitihada zaidi za
kupambana dhidi ya janga hili la UKIMWI kwa kuandaa mpango, mkakati unaolenga
na kuhimiza mwitiko shirikishi katika sekta ya kinga, matunzo, matibabu na
kupunguza athari zitokanazo na ukimwi ambapo mpango huo unatarajia kufanyika
kwa miaka mitatu kuanzia Julai 2014 mpaka Juni 2017 katika Halmashauri zote kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali.
Na
kwa upande wa wadau walisema lengo la semina hiyo shirikishi ni kusambaza
matokeo ya tafiti za Asasi na wadau wanaofanya kazi na vijana hivyo matarajio
yao ni washiriki wote katika mkutano huo watumie taarifa hizo katika mipango
kazi yao pia waboreshe huduma kulingana
na taarifa hizo.
NA
DIANA BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM, IRINGA
Post a Comment