JESHI
la majini la Australia limekamata na kuharibu kilo 353 za madawa ya
kulevya aina ya heroin yenye thamani inayokadiriwa kuwa zaidi ya dola
milioni 700 katika pwani ya Tanzania.
Askari
wa meli ya HMAS Melbourne waliyagundua madawa hayo katika meli moja
Jumatano iliyopita wakiwa katika shughuli za kupiga vita ugaidi na
kuimarisha usalama maeneo ya baharini Mashariki ya Kati na Bahari ya
Hindi.
Mkuu
wa kikosi hicho, Daryl Bates, alisema hatua hiyo ilikuwa ni pigo katika
kukwamisha njia za kupatikana kwa fedha zinazotumiwa na magaidi.
Credits: AFP
Post a Comment