Kamishna
wa Magereza nchini Zambia Percy Chato (wa nne kulia) akiwa na
Jenerali wa Magereza Tanzania John Minja (katikati) wakimsiliza kwa
makini Mnadhimu wa Jeshi la Magereza Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mmeta
Manyara akijitambulisha. Kamishna Chato ametembelea Makao Makuu ya
Magereza ikiwa kni ziara ya siku sita nchini Tanzania.Wa tatu kulia ni
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza John Yumbe, wa pili kulia ni
Kamishna Msaidizi wa Magereza Tebuho Nyambe na wa kwanza ni Mrakibu
Msaidizi wa Magereza James Nkoloma wote kutoka Makao Makuu ya Magereza
nchini Zambia.
Kamishna
wa Magereza nchini Zambia Percy Chato ( wa nne kushoto), akipokea
taarifa fupi kutoka kwa mmoja wa maofisa kiwandani Ukonga. Kamishna
Percy alitembelea Kiwanda cha Magereza Ukonga, Dar es salaam kuona
shughuliza za urekebishaji wa wafungwa zinavyofanyika.
Kamishna
wa Magereza nchini Zambia Percy Chato akisaini kitabu cha wageni
Kiwandani Ukonga, wa pili kushoto ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa
Magereza nchini Tanzania Dkt Juma Ali Malewa.
Kamishna
wa Magereza nchini Zambia Percy Chato (katikati) akifurahia kukaa
katika moja ya samani zinazotengenezwa kiwandani Ukonga, kushoto ni
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza Tanzania, Dkt Juma Ali
Malewa na kulia ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza wa Zambia
John Yumbe.
Kamishna
wa Magereza nchini Zambia Percy Chato (wa pili kulia) akiangalia samani
maridadi kabisa zinazotengenezwa kiwandani Ukonga ikiwa ni sehemu ya
huduma ya urekebishaji wa wafungwa kwa vitendo
Kamishna
wa Magereza nchini Zambia Percy Chato wa (pili kushoto) akipokea
maelezo kutoka kwa mmoja wa mafundi katika Karakana ya magari ya
Magereza iliyoko Ukonga Dar es salaam, wa kwanza kulia ni Kamishna wa
Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini Dkt Juma Ali Malewa.
Kamishna
wa Magereza nchini Zambia Percy Chato (mwenye suti) akipokea salaam ya
heshima kutoka kwa Paredi maalum (halipo pichani) lililoandaliwa maalum
kwa jairi yake katika uwanja wa paredi wa Chuo Cha Maafisa wa Magereza
Ukonga.Nyuma yake ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini
Dkt Juma Ali Malewa na mwenye nguo za kijani ni Kaimu Mkuu wa Chuo
Kamishna Msaidizi wa Magereza Erasmus Kundi.
Kamishna
wa Magereza nchini Zambia Percy Chato (mwenye suti) akikagua paredi
maalum lililoandaliwa kwa heshima yake katika Chuo cha Maafisa wa
Magereza Ukonga, Dar es salaam.
Askari
wa Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani (KMKGM) cha Ukonga
jijini Dar es salaam wakionesha aina mbalimbali za mzoezi ya kujihami na
kuanguka bila kuumia katika kukabiliana na hatari yoyote, mblele ya
Kamishna wa Magereza nchini Zambia Percy Chato
Kamishna
wa Magereza nchini Zambia Percy Chato (katikati) akifurahia "juice" ya
madafu aliyoandaliwa katika viwanja vya Garden Ukonga Dar es salaam wa
pili kushoto ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza Nchini Dkt.
Juma Ali Malewa na wa Kwanza kulia ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Magereza nchini Zambia John Yumbe kwa pamoja wakifurahia "juice" ya
madafu.
kamishna
wa Magereza nchini Zambia Percy Chato akipokea maelezo kutoka kwa mmoja
wa maofisa wa Kikosi Maalum cha KMKGM jinsi ya kujiandaa ktuliza ghasia
magerezani au popote pale itakapohitajika. Picha zote na Insp. Deodatus
Kazinja wa Magereza.
Post a Comment