WINGA Gareth Bale ameendelea kung'ara Real Madrid akiiwezesha timu hiyo kutanguliza mguu mmoja Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya kufuatia ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya wenyeji Schalke usiku huu.
Mchezaji huyo ghali duniani aliyenunuliwa kwa Euro Milioni 86, alifunga mabao mawili na kutoa pasi mbili za mabao katika ushindi huo mnono.
Kocha Carlo Ancelotti amevutiwa na kiwango cha Bale na akamwagia sifa baada ya mechi hiyo ambayo mabao mengine Real yalifungwa na Karim Benzema na Cristiano Ronaldo kila mmoja mawili pia huku bao la kufutia machozi la wenyeji likifungwa na Klaas-Jan Huntelaar.
Sisi noma; Ronaldo kulia na Bale kushoto wakishangilia moja ya mabao yao usiku huu Real ikishinda 6-1 dhidi ya Schalke |
Msituni: Winga wa Real Madrid, Gareth Bale akipasua katikati ya msimu wa wachezaji wa Schalke
Post a Comment