Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA OFISI YA IECO UKANDA WA AFRIKA JIJINI DAR

 


01
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akikata utepe kufungua rasmi ofisi ya IECO ukanda wa Afrika, yenye makao yake makuu Beijing China iliyofunguliwa jijini Dar es Salaam  Tanzania, leo Feb 5, 2014 kwa ajili ya kuwakilisha nchi za Afrika na tayari imeanza mchakato katika kukabiliana na magugu maji katika Ziwa Viktoria sambamba na shughuli nyingine zinazolenga utunzaji mazingira na namna ya kukabiliana na majanga yanayotokana na athari za tabia nchi. Kulia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka. Picha na OMR
02
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia Sola Pawa ndogo maalum kwa kuchajia simu na kusomea baada ya kufungua rasmi ofisi ya IECO ukanda wa Afrika, yenye makao yake makuu Beijing China iliyofunguliwa jijini Dar es Salaam  Tanzania, leo Feb 5, 2014 kwa ajili ya kuwakilisha nchi za Afrika. Kushoto ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka. Picha na OMR

03
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akikabidhiwa Nembo ya Taasisi hiyo iliyofunguliwa jijini Dar es Salaam, leo. Picha na OMR
05 
Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akiagana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka, baara ya uzinduzi huo. Picha na OMR
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top