Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAKAO MAKUU YA CHADEMA YANUSURIKA KULIPULIWA



Kumekuwa na jaribio la kulipua Ofisi za Makao Makuu ya CHADEMA, Mtaa wa Ufipa, Kinondoni majira ya saa 8 usiku wa leo Februari 11.

Maelezo ya awali yanaonesha kwamba watu waliofanya tukio hilo walifika maeneo ya ofisi wakiwa na gari ndogo ambayo plate number zake zilikuwa zimezibwa.


Wakapaki kama vile wanaendelea na shughuli kwenye 'ofisi' nyingine iliyo jirani na Makao Makuu, kisha mmoja wao akatoka nje ya gari na kuelekea kwenye hiyo ofisi ya jirani.



Gari lile liliendelea kuwa pale kwa muda hadi walinzi walipoanza kulishuku na kulifuatilia, ghafla mmoja aliyekuwa ndani ya gari akasikika akisema 'tayari...twende zetu...', aliyekuwa ameshuka kwenye gari kumbe alikuwa ana-guard wenzake waliokuwa wakiwasha moto.

Wakati walinzi wanaanza kuwafuata kuchukua hatua za kuwadhibiti, gari lile likaondolewa kwa kasi huku likimkosa kosa kumgonga mtu mmoja.

Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama, ALIYEWAHI KUKAMATWA AKIPANGA UGAIDI Wilfred Muganyizi Lwakatare anasema kwa namna tukio hilo lilivyoendeshwa, lilikuwa na malengo ya kulipua Ofisi za CHADEMA Makao Makuu.

Tukio hilo limetolewa taarifa polisi.

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top