Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi kadi ya CCM kwa mwanachama mpya
wa Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Asha Chadenje aliyehama kutoka Chama Cha
Wananchi,CUF wakati wa sherehe za uzinduzi wa sherehe za kutimiza miaka
37 ya chama hicho zilizofanyika kimkoa huko Kiwalala, wilayani Lindi
Vijijini.
Mke
wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mama Salma Kikwete
akimpongeza aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo, CHADEMA, Mkoa wa Lindi Bwana Ali Omar Chitanda, ambaye
amekihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi. Mama Salma
baada ya kumpongeza alimtambulisha kwa wananchi akiwa pamoja na Bi. Asha
Chadenje wakati wa sherehe za uzinduzi wa miaka y37 ya CCM mkoani
Lindi.
Mke
wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi
anayewakilisha Wilaya ya Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akimnadi Mgombea
wa Udiwani wa Kata ya Kiwalala kupitia CCM, Bwana Shineni Hamis Zahoro
wakati wa sherehe za miaka 37 ya Chama Cha Mapinduzi zilizofanyika
kimkoa katika kijiji cha Kiwalala terehe 1.2.2014.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia mamia ya wanachama wa CCM na
wananchi wa Lindi Vijijini wakati akizindua rasmi sherehe za kutimiza
miaka 37 ya Chama Cha Mapinduzi katika mkoa wa Lindi. Shughuli hiyo
ilifanyika katika kata ya Kiwalala iliyoko Lindi Vijijini. Sherehe hiyo
ilienda sambamba na kumnadi mgombea wa udiwani kupitia Chama Cha
Mapinduzi katika kata hiyo Bwana Shineni Hamis Zahoro katika uchaguzi
unaotarajiwa kufanyika tarehe 9.2.2014.
Ngoma
ya Tambiko inayochezwa na wananchi wa kabila la wamakonde nayo ilikuwa
ni kivutio tosha wakati wa sherehe za uzinduzi wa miaka 37 ya Chama Cha
Mapinduzi zilizofanyika kimkoa kwenye kata ya Kiwalala, Lindi Vijijini
tarehe 1.2.2014. PICHA NA JOHN LUKUWI


Post a Comment