Mambo matano Yatakayokugusa katika maisha ya Diamond Platnumz
01. Diamond Platnumz aliachwa na baba yake
Diamond alizaliwa tarehe 2, October mwaka 1989 katika Hospitali ya
Amana Dar es salaam. Akiwa na umri mdogo wazazi wake walitengana na baba
yake kumuacha bila msaada wowote. Hapa chini huyo ndiyo baba yake
diamond.
02. Chumba kupangishwa ili kumsomesha
Baada ya wazazi wake kutengana, Diamond aliamia kwa bibi yake huko
tandale na ilipofika muda wa yeye kwenda sekondari ilibidi bibi yake
apangishe chumba kimoja ili Diamond aende shule na ikabidi alale chumba
kimoja na bibi na mama yake.
03. Aliacha shule kwa kukosa Ada
Diamond alikua na akili darasani na
alipomaliza elimu yake ya O’level
ilikosekana pesa ya kumpeleka A’level na hapo ndio ilikua mwisho wa
elimu yake.
04. Diamond ameshafanya kazi viwandani, Kafanya kazi za kupigisha simu , kuuza mitumba na kuuza maji.
Kuna kipindi Diamond alikuwa akifanya kazi katika kiwanda cha mabegi
kilichoko Mikocheni na kulipwa mashahara wa shilingi 2,000 kwa masaa 8.
05. Mama yake alisaidia sana kutoka kwake
Mama yake alikuwa anampeleka kwenye talent show na kumsubiria hadi
usiku mpaka aperform ndo wanarudi wote. Ndugu zake wengine waliona
anamdekeza mwanae.
Post a Comment