“Mabadiliko katika mfumo wa Serikali katika utendaji kazi kupata mafanikio haraka"
Ofisi ya
Rais - Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi (OR- UUM) imetoa taarifa kwa
umma kuwa utekelezaji wa mfumo wa – Big Results Now ! (BRN) unaendelea
vizuri. Mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) unaweka utaratibu thabiti wa
kufuatilia na kutathimini utekelezaji wa miradi katika maeneo sita ya
kimkakati kitaifa (Kilimo, Elimu, Maji, Nishati , Uchukuzi na Utafutaji
wa Rasilimali). Mfumo wa BRN unaweka wazi malengo pamoja na kuainisha
uwajibikaji kwa kila mshiriki mmoja au taasisi katika utekelezaji wa
miradi ya Serikali ili kupata mafanikio haraka.
Kila
Wizara inayotekeleza mfumo huu imeanzisha Kitengo cha Kusimamia
Utekelezaji (Ministerial Delivery Unit (MDU)) ambacho kinafanya kazi kwa
karibu sana na OR-UUM. Majukumu ya MDU ni kufuatilia na kuthamini
utekelezaji wa miradi wa kila siku na kuanda taarifa za utekelezaji za
kila wiki na mwezi ambazo huwasilishwa OR-UUM. Taarifa za MDU
zinajadiliwa kila mwezi kwenye mikutano ya Kamati ya Wizara ya Kusimamia
eneo la kimkakati Kitaifa (Steering Committee Meetings) ambayo
Mwenyekiti ni Waziri wa Wizara husika pamoja na Baraza la Mageuzi na
Ufuatiliaji Utekelezaji ambalo Mwenyekiti ni Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania. Mikutano hii inalenga kutatua changamoto au vikwazo
vilivyojitokeza.
Aidha,
Serikali ipo katika mchakato wa kuanzisha Vitengo vya Kusimamia
Utekelezaji katika ngazi za Mikoa (Regional Delivery Units - RDUs)
pamoja na Mamlaka za Serikali za Mitaa (Council Delivery Units - CDUs)
ili kuongeza ufanisi wa kutekeleza miradi katika ngazi zote.
Bwana
Omari Issa, Mtendaji Mkuu wa OR- UUM alisema, “Tanzania ina mawazo
makubwa na Dira na mipango sahihi ya kuleta maendeleo. kinachokosekana
ni mfumo sahihi wa kufuatilia utekelezaji ili kupata matokeo
yaliyolengwa. BRN inaondoa dosari hii. Aidha, BRN inaleta mageuzi ya
uwajibikaji katika ngazi zote za utumishi wa umma.
Ili
kufanikisha BRN, tunahitaji kupata ushirikiano kutoka sekta binafsi
ambayo italeta teknolojia, utaalum wa menejimenti na mtaji. Ili
kuhamasisha ushiriki wa sekta binafsi, BRN imeanza mchakato wa
kurazinisha mfumo na taratibu za ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta
Binafsi (PPP) ili tuhakikishe kwamba sekta binfasi inatoa mchango wake
stahiki katika kutekeleza BRN



Post a Comment