Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MSANII MAARUFU WA ENDLESS FAME AFUNGUKA KUHUSU BOSI WAKE WEMA SEPETU LIVE!!


 


Msanii wa kampuni ya Endless Fame Films ya Wema Sepetu, Mirror amesema, Wema ni kama dada yake na wanaishi kama watu wa familia moja na kwamba tetesi za kuwa wana uhusiano wa kimapenzi hazina ukweli wowote.



“Hapana, hakuna kitu kama hicho kabisa,” Mirror ameiambia Bongo5 kukanusha tetesi hizo.

“Uhusiano ni kama msanii na bosi wake, she is like a sister kwangu, tunaheshimiana, hizi romance na vitu vingi havipo,” ameongeza.

Mirror amemuelezea Wema kama bosi mwenye roho nzuri.

“Napenda jinsi alivyo, ana roho nzuri, naishi naye poa, nina shida namuelezea, ana kitu chake tunakaa tunaongea, we have fun, we live like a family.”

Mirror amesema tangu ajiunge na kampuni hiyo, mabadiliko ni makubwa katika muziki na maisha yake. “Napata show nyingi, napata connection kufahamiana na watu,”amesema Mirror.

Msanii huyo wa Baby, amesema kwa sasa amefanya remix ya wimbo wake ‘Nadata na Wewe’ aliomshirikisha Diamond na mwingine amepanga kumshirikisha Diamond Platnumz.

~Bongo5.com
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top