kamanda-Justus-Kamugisha
MTUHUMIWA
wa mauaji ya watu tisa na unyang'anyi wilayani Tarime mkoani Mara,
aliyekuwa akihojiwa Polisi kwa tuhuma zilizokuwa zikimkabili, amefariki
dunia katika Hospitali ya Wilaya wakati akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa
pumu. Kamanda wa Polisi Tarime na Rorya, Kamishina Msaidizi Justus
Kamugisha, alisema kuwa mtuhumiwa huyo jina lake halisi ni Charles
Kichune (38) na alifariki usiku wa kuamkia jana wakati akitibiwa ugonjwa
huo hospitalini.
Majina mengine aliyokuwa akiyatumia kwa mujibu wa Kamanda Kamugisha ni pamoja na Josephat Chacha na Charles Msongo.
"Mwili
wa marehemu upo chumba cha maiti katika Hospitali ya Wilaya ukisubiri
kufanyiwa uchunguzi na kuchukuliwa na ndugu zake,” alisema Kamanda
Kamugisha.
Baadhi
ya raia waliouawa ni pamoja na David Yomami, Samuel Matiko, Robert
Machumbe, Zakaria Marwa , Juma Nyaitara, Juma Mwita, Marwa Mwita na
Erick Makanya.
Kwa
mujibu wa maelezo ya Kamanda Kamugisha, Kichune baada ya kukamatwa
alikiri Polisi kuhusika katika mauaji ya watu mbalimbali katika kata za
Binagi, Turwa na Kitare katika vijiji vya Mogabiri, Kenyamanyori, Nkende
na Rebu.
Kamanda
Kamugisha alisema mtuhumiwa huyo Kichune alikamatwa Februari 6 mwaka
huu mkoani Tanga baada ya Polisi kufuatilia mtandao wake baada ya kupata
taarifa kutoka kwa raia wema.
Baada
ya kukamatwa, uchunguzi wa Polisi ulibaini kuwa baada ya mauaji ya watu
tisa, mtuhumiwa alikodisha pikipiki kutoka kijiji cha Kenyamanyori
alikokuwa akiishi, hadi Musoma.
Alipofika
Musoma, inadaiwa alihifadhi bunduki aina ya SMG na risasi kadhaa kwa
mshirika wake, Marwa Keryoba maeneo ya Bweri na alipokamatwa alimtaja
Keryoba kuwa ndiye anayetunza silaha hiyo. Februari 7 mwaka huu, Polisi
walifuatilia silaha hiyo kwa Marwa na kumkuta mtuhumiwa, ambapo
alitakiwa kujisalimisha lakini alikaidi na kuanza kurushia risasi
askari.
“Marwa
aliuawa Februari 7 alfajiri Bweri Musoma, wakati alipotakiwa
kujisalimisha na kukaidi na kuanza kurushiana risasi na askari," alisema
Kamanda Kamugisha. *Mtuhumiwa mwingine Kwa mujibu wa Kamanda Kamugisha,
kuna mtuhumiwa mwingine sugu wa mauaji ya watu zaidi ya 10, Senso
Magabe ameuawa katika majibishano na Polisi wiki iliyopita.
Hata
hivyo katika majibishano hayo, wenzake watatu walifanikiwa kutoroka na
msako unaendelea wilayani hapa ambapo wananchi wameombwa kutoa
ushirikiano Polisi ili kufanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao.
Kamanda
Kamugisha alisema tayari watu wanne waliokuwa katika mtandao huo wa
ujambazi wamefikishwa mahakamani kwa mashitaka ya unyang'anyi na mauaji.
Watuhumiwa
waliofikishwa mahakamani ni pamoja na Kyoma Manguh, Marwa Mwita ,
Yohana Mgosi na Chacha Bugichere ambapo kesi zao zitatajwa Februari 19
mwaka huu.
Jana
mamia ya wananchi wilayani Tarime walifurika kuona mwili wa Kichune
maarufu Kenonke ambaye amekuwa tishio kwa wakazi wa wilaya hiyo. Polisi
imetangaza zawadi ya Sh milioni moja kwa atakayetoa taarifa
zitakazofanikisha kukamata silaha za moto katika wilaya za Tarime na
Rorya.Chanzo Mwananchi Online
Post a Comment