MZEE MALECELA NA PAUL MAKONDA WAOMBE RADHI KWA VIONGOZI WA DINI
0.1 Kitendo alichokifanya hivi
karibuni Ndugu Paul Makonda Katibu wa Chipukizi na Uhamasishaji pale
alipoongea na vyombo vya Habari pamoja na mambo mengi aliyoyaongea kubwa
zaidi ni alipotamka wazi kwa kuwatuhumu baadhi ya Viongozi wa Dini kwa
kutoa maneno ya kejeri na dharau dhidi yao kuwa “MASHEIKH NA MAASKOFU
WAKIWEMO NA VIJANA WANAOTAKA FEDHA ZA BURE WAENDE KWA EDWARD LOWASA”
kitendo ambacho hakuwatendea haki wala adabu Viongozi hawa wa Dini.
Kitendo hicho cha kuwakejeri na kuwadhalilisha ni utovu wa Nidhamu wa
hali ya juu sana, kwani kauli aliyoitoa kila Muumini ilimshitua sana,
kwani ni kauli haikupaswa kutolewa na Kiongozi wa Vijana aliyekuwa
katika nafasi Muhimu ya Uongozi wa Jumuiya Kitaifa, kwani kauli yake
hiyo yenye ukakasi wa hali ya juu sana imempa kichefuchefu kila mmoja
anaewaheshimu Viongozi wa Dini, kwani Viongozi wa Dini wanaheshima zao
binafsi na kuheshimika Duniani kote na mpaka Serikali huwaomba Viongozi
wa Dini kushiriki pamoja kutatua na kushauriana katika maswala
mbalimbali yanayoizunguka jamii.
Kauli hiyo ni nzito sana aliyoitoa Ndugu Paul Makonda sio ya kuipuuza
hata kidogo na kuicha hivi hivi nina muomba kwa Heshima na taadhima
Mwenyekiti wa Vijana wa Taifa awathibitishie Watanzania kuwa kauli
aliyoitoa Ndugu Paul Makonda ni ya Umoja wa Vijana au ni yake binafsi.
Kwani mimi binafsi nimekuwa katika Umoja wa Vijana kama Mwenyekiti wa
Vijana Mkoa wa Shinyanga mstaafu na Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa
Vijana Taifa lakini pia Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Umoja wa Vijana
Taifa, nafahamu kauli au matamko mazito kama yaliyotolewa na Ndugu Paul
Makonda hutolewa na Mkutano mkuu wa Taifa, Mkutano wa Baraza Kuu Taifa
na hata kamati ya Utekelezaji Taifa.Mimi siamini kama hiyo ni Kauli ya
Umoja wa Vijana kwa kadri ninavyofahamu utaratibu ndani ya Jumuiya na
Chama kwa ujumla, sasa tunajiuliza huyu kijana kauli hizi nzito nzito
ambazo hazilingani na umri wake na wala hadhi ya kiuongozi aliyonayo
anazitowa wapi huenda tunaamini kuna kundi au genge la mahafidhina liko
nyuma yake lililoamua kumtumia aidha kwa kujua au kwa kutokujua.
Jambo jingine muhimu alitutuhumu pia sisi yani mimi Khamis Mgeja,
Mzee Mgana Msindai na Ndugu John Guninita kuwa alidai t--------- na
Ndugu Edward Lowasa, tuhuma hizi si za kweli hata kidogo napenda
Watanzania wafahamu tuhuma zote mbali mbali ambazo kijana huyu amekuwa
akitushutumu si za kweli na ni za kipuuzi ninaiomba jamii kumpuuza kwani
Ndugu Makonda bado mchanga kisiasa anatafuta umaarufu kwa kasi kwa
kutumia migongo yetu sisi wakongwe kisiasa, kwani sisi aliotutuhumu
atambue sisi ni wakongwe na ni Magwiji katika siasa za kiungwana hapa
Tanzania, tunauwezo wetu binafsi wa kufikiri na kuamua kile
tunachokiamini kwa maslahi ya Chama na Taifa kwa ujumla, kwa ujumla
tunataka Ndugu Paul Makonda na washirika wake waache kelele ambazo
wamekuwa wakilalamika mara kwa mara hii ni dalili ya kuelemewa ndio
maana hawaishi kumsemasema na kumkejeri Ndugu Edward Lowasa wakati
ambapo jamii inamuona kuwa ni mtu wa msaada mkubwa katika kuchagiza
maendeleo kwa kushirikiana na jamii. Kijana Makonda atambue sisi
tumewekeza jasho jingi katika chama hiki na kamwe hatutokubali
kudhalilishwa na kijana mchanga wa kisiasa kama huyu, pia kama ni
kuwekeza jasho sisi tuna debe ishirini yeye hata robo hajafikisha katika
medani za kisiasa kwa hivyo anafanya maajabu ya kisiasa ni maajabu ya
panya kufukuza paka na anacheza ngoma asiyoijuwa.Pia jamii inamuona
Ndugu Edward Lowasa ni mtu muungwana, mwenye uwezo mkubwa wa kiutendaji,
mwenye ushauri na ushawishi mkubwa katika machangizo ya maendeleo, sifa
kubwa nyingine ya ziada ni uvumilivu na hasa kuwavumilia watu wenye
kumrushia madongo kama Paul Makonda na genge lao la mahifidhina.
Kuhusu kauli aliyoitamka Ndugu Makonda ya kwamba Ndugu Edward Lowasa
hawezi kuwa Rais kauli hii imetoa picha ya kuyajuwa yaliyofichika katika
fikra za kundi hili la wahifidhina lakini pia watambue maamuzi yote
hufanywa na Vikao halali vya chama na jumuiya zake, na wakati ukifika
vikao vitaamua na si Makonda na marafiki zake.
0.2 MZEE MALECELA KUPONGEZA KAULI ZA KASHFA DHIHAKA NA KEJERI DHIDI
YA VIONGOZI WA DINIKufutia tukio la hivi karibuni la kijana Paul Makonda
kutoa maneno ya kashfa kejeri na dhihaka dhidi ya viongozi wa Dini,
baadhi ya wanasiasa na vijana maaajabu makubwa kutokana na kauli hizo za
Makonda tumemshangaa Mzee Malecela kuibuka na kuunga mkono na
kumpongeza kijana huyu mtovu wa nidhamu.
Tulitegemea kila Mtanzania kwamba baada ya kauli hizo Mzee Malecela
angeibuka na kumuongoza njia sahihi na kumpa ushauri kijana huyu
aliyepotea kimaadili wa kwenda kuwaomba radhi na kuwaangukia viongozi wa
Dini, ndugu Edward Lowasa, Ndugu Khamis Mgeja, Ndugu Mgana Msindai,
Ndugu John Guninita ikiwemo na vijana kwa ujumla.Maajabu makubwa jambo
ambalo Watanzania hawakutegemea jinsi wanavyomfahamu Mzee Samwel
Malecela na heshima yake, tulitaraji kuwa Mzee angemkemea kijana huyu
mtovu wa Nidhamu badala yake anampongeza na kumuunga mkono na kuwataka
Watanzania wamuunge mkono kwa kauli zake za utovu wa Nidhamu ambazo
hazina tija kwa Chama na maendeleo ya Taifa kwa ujumla, pia katika
maajabu mengine Mzee Malecela alimshambulia mwanachama mwenzake Ndugu
Edward Lowasa kwa kumtuhumu kwa tuhuma nyingi mbalimbali ambazo hana
ushahidi nazo.Mzee Malecela amesahau huko nyuma yeye alishawahi
kutuhumiwa kuwa alipewa fedha kutoka nchi za uarabuni na mpaka
kubadilisha dini na kuitwa jina la JUMANNE ili aungwe mkono kupewa nguvu
za kugombea Urais.
Kuhusu uchu wa Urais anaomtuhumu Ndugu Lowasa amesahau yeye ndiye ana
uchu mkubwa sana wa Madaraka alikuwa akiomba nafasi za ndani ya Chama
haswa kwa kiti cha Urais kwa awamu mbalimbali akaonekana hafai na
hatoshi na mpaka jina lake likawa halipitishwi na chama baada ya
kumgundua ni dhaifu na anakasoro kubwa za kimaadili na mpaka ikapelekea
Baba wa Taifa akachoka kumvumilia na hatimae alimtungia kitabu “UONGOZI
WETU NA HATIMA YA TANZANIA” hii ni kuonyesha kuwa Mzee Malecela alikuwa
sugu wa matatizo yaliyokuwa yakikiuka maadili.Jambo jingine alilokuwa
nalo la uchu wa madaraka Mzee Malecela ni pale alipong’ang’ania kiti
chake cha ubunge bila kujali umri wake na wananchi wa jimbo la Mtera
ilifika mahala walimchoka baada ya kugundua anasinzia Bungeni na kwenye
jimbo laketulishuhudia Kibajaji kikiliangusha Katapila maana yake
aliangushwa ubunge na mtoto mdogo Mhe Livingstone Lusinde.Jambo jingine
Mzee Malecela ameshindwa kutambua wanaokivuruga chama ni wale
wanaozungumza nje ya vikao halali vya chama na jumuiya zake na kuyageuza
kuwa ndio msimamo wa chama au jumuiya.
Kwa hivyo Mzee Malecela kuendelea kutushambulia hatutendei haki kwani
hakuna shughuli yoyote ya chama iliyokwama kuanzia ngazi ya tawi hadi
taifa kwa sababu yetu sisi.NINAPENDA KUTOA USHAURI KWA MZEE MALECELA,
MAKONDA NA WATANZANIA WENZANGU KWA UJUMLA, Tanzania kama taifa tumefika
pabaya kwani kila mmoja amebaki kuwa mlalamikaji na kutuhumiana
pasipokuwa na ushahidi hili jambo ni hatari kwa mustakbali wa nchi kwani
hivi sasa baadhi ya watu wanamgeuza Ndugu Edward Lowasa kuwa ni agenda
ya kitaifa huku wakiacha mambo muhimu ya nchi na maisha ya
watanzania.kwani tulitegemea wazee wetu kama kina Mzee Malecela
watushauri vipi taifa linaweza kukabiliana na changamoto zilizopo hivi
sasa kwa mfano deni la taifa, mchakato wa Katiba Mpya, matatizo ya
umasikini, tatizo la ajira kwa vijana, hombwe kubwa kuwahi kutokea baina
walionacho na wasionacho, mauaji yanayotokea sasa maeneo mbalimbali
kati ya wakulima na wafugaji ikiwemo kuchomeana nyumba, mauaji ya
kikatili kule Tarime na maeneo mbalimbali nchini, ajali mbali mbali za
barabarani zinazouwa nguvu kazi ya Taifa, tatizo kubwa la rushwa,
uporaji wa rasilimali za Taifa na ujangili wa kutisha, Tanzania kutumika
kama korido la kupitishia madawa ya kulevya na binadamu, oparasheni
tokomeza, wananchi kujichukulia sheria mkononi, ubadhilifu wa mali za
umma haswa ukizingatia ripoti ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali na
taarifa za kamati mbalimbali za bunge, jambo jingine kubwa lilipo kwa
sasa ni kuhusu rasilimali ya gesi iliyovumbuliwa kwa wingi nchini wakati
taifa lipo katika mchakato wa kutunga sera na sheria ya gesi na mafuta.
Mzee Malecela na wenzake hayo yaliyotajwa hapo juu ndio mambo muhimu
yanayogusa nchi na sio mtu Lowasa Lowasa Lowasa tulitegemea atushauri
Tanzania kama taifa tufanye nini Watanzania kwa kushirikiana na Serikali
yetu kwani matatizo hayo yanahitaji ushirikishwaji baina ya wananchi na
Serikali yao, Watanzania wangeyapata hayo kupitia uzoefu wake kama
alivyowahi kuwa Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Makamu wa Mwenyekiti wa CCM
kuliko maajabu ya kuonyesha Flana yenye maneno ya “FRIENDS OF LOWASA”
kuwa kama ndio tatizo la Taifa.
Mzee Malecela kuwaonyesha Watanzania Flana ya Lowasa ndio tatizo la
taifa hii inaonyesha wazi Mzee amechoka na amefilisika kifikra na
anazeeka vibaya ninapenda nimpe ushauri wa bure Mzee wangu atulie alinde
heshima yake.Pia napenda nitoe ushauri kwa Mzee Malecela, Paul Makonda
pamoja na washirika wao wasome alama za nyakati na waangalie mahitaji ya
siasa kwa sasa na waone Watanzania wanamuhitaji Kiongozi wa namna gani
wa Tanzania ya kesho, ninawaomba wakubali yaishe wasije
kupinganaTanzania na nguvu ya umma na upepo wa kisisa kwa sasa na pia
watambue mpaji ni MUNGU alitakalo MUNGU hakuna mwanadamu atakaelizuia.
NAWATAKIA KILA LA HERI KATIKA UJENZI WA TAIFA
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WABARIKI WATANZANIA
TAARIFA HII IMETOLEWA NA NDG KHAMIS MGEJA
…………………………………………….
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WABARIKI WATANZANIA
TAARIFA HII IMETOLEWA NA NDG KHAMIS MGEJA
…………………………………………….


Post a Comment