Naibu
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Jenista Mhagama (MB)
akikaribishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa
Elimu ya Juu Bw. George R.W. Nyatega (kushoto)) katika Ofisi za Bodi
hiyo zilizoko Mwenge, Dar Es Salaam .
Mh.Naibu Waziri akipeana mkono na baadhi ya wawakilishi wa Menejimenti ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.
Naibu
Waziri Mhe. Jenista Mhagama (kushoto) wakiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Bw. Nyatega, wakifuatilia
mada ya Utoaji Mikopo iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Uchambuzi na
Utoaji Mikopo Bw. Onesmus Leizer (hayupo pichani)
![]() |
Naibu
Waziri alipata pia bahati ya kukutana na mmoja wa wanafunzi wake Bi.
.Sarah Fihavango ambaye kwa sasa ni Afisa Mikopo Mwandamizi wa Bodi ya
Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.
----------
Naibu
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Jenista Mhagama (Mb)
ametembelea ofisi za makao makuu ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu
ya Juu yaliyopo barabara ya Sam Nujoma Mwenge Dar Es Salaam.
Ziara
hiyo inafuatia uteuzi wake uliofanywa hivi karibuni na Mhe. Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.
Mhe.Jenista
Mhagama(Mb), ameipongeza Menejiment ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa
Elimu ya Juu kwa utendaji wao wenye ufanisi ulioperekea migomo kupungua
katika vyuo mbali mbali nchini, aidha Naibu Waziri amepongeza pia
jitihada za Bodi ya Mikopo inayofanyika katika urejeshwaji ambayo
imeperekea kupatikana kwa Bilioni 19, ambazo pia zimetumika katika
ukopeshaji wa Wanafunzi wahitaji katika mwaka wa masomo 2013/14.
Katika ziara hiyo Mhe. Naibu Waziri aliambatana na Mkurugenzi wa Elimu ya Juu, Prof. Sylivia Temu.
Akimtambulisha
Naibu Waziri kwa Menejimenti ya Bodi ya Mikopo, Mkurugenzi Mtendaji wa
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Bw. George Nyatega alisema
``……ni bahati kutembelewa na Naibu Waziri ambaye bado ni mpya kwenye
Wizara, kwani ni majuzi tu ndiyo Mhe. Mhagama ameteuliwa katika Wizara
hii’’.
Aidha,
Bwana Nyatega alitumia fursa hiyo kumwelezea Naibu Waziri shughuli za
kila siku za Bodi ya Mikopo ikiwa ni pamoja na historia fupi ya
kuanzishwa kwa Bodi ya Mikopo, mafanikio, na changamoto zinazoikabili
Bodi hiyo.
Michuzi Media group
Michuzi Media group







Post a Comment