Naibu
Waziri wa Maji, Amos Makalla akisikiliza ripoti ya maji ya Wilaya ya
Morogoro katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, kushoto ni Mbunge
wa Morogoro Kusini, Innocent Kalogeris.
Mbunge
wa Morogoro Kusini-Mashariki, Lucy Nkya akizungumza katika mkutano wa
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla wilayani Morogoro. .
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Amanzi akizungumza katika mkutano wa Naibu Waziri wa Maji katika ziara yake wilayani hapo
Mbunge
wa Morogoro Kusini, Innocent Kalogeris akizungumza na wakazi wa kijiji
cha Bwira Chini katika ziara ya Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla
katika jimbo lake, wilayani Morogoro.
Naibu
Waziri wa Maji, Amos Makalla akizungumza na wananchi wa Bwira Chini
katika ziara yake kijijini hapo, kushoto ni Mbunge wa Morogoro Kusini,
Innocent Kalogeris na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Amanzi.
Wakazi
wa kijiji cha Bwira Chini wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maji, Amos
Makalla (hayupo pichani), wakati wa alipotembelea kijiji hicho katika
ziara yake wilayani hapo.
………………………………………………………………………………………………….
Naibu
Waziri wa Maji, Amos Makalla ameanza ziara yake mkoani Morogoro
Jumatano kwa kutembelea Mamlaka ya Mazingira na Majisafi Morogoro
(MORUWASA).
Mhe.
Makalla alifika MORUWASA na kujionea utendaji na kupata taarifa ya
mamlaka hiyo ambayo inatoa huduma ya maji mjini Morogoro na kukagua
miradi inayotekelezwa mkoa huo.
“Ninawaagiza
wakandarasi wahakikishe wanarudi kwenye maeneo yao ya kazi mara moja,
kama Waziri Maghembe alivyoagiza. La sivyo Serikali itaangalia taratibu
na kuchukua hatua kali. Na mkandarasi atayekaidi hatapata kazi sio tu
Wizara ya Maji, bali Tanzania nzima”, alionya Naibu Waziri.
“Muwe
karibu na kuwahudumia vizuri wateja na kuwe na ratiba nzuri ya mgao na
ya kueleweka na kwenye dharura mfike mara moja bila kuchelewa. Muondoe
urasimu usio wa lazima katika kutoa huduma kwa wananchi wote”, alisema
Makalla.
Pia,
alisema wananchi waiunge mkono Serikali katika kutunza mazingira na
vyanzo vya maji na amekuja Wizara ya Maji kutimiza sera za maji na
mipango ya Serikali katika sekta hiyo na si vinginevyo. Na kuahidi
kuwasilisha maombi yote aliyoyapokea Wizarani na kuyapapa msukumo
yafanyiwe kazi, isipokuwa yale yaliyo ndani ya uwezo wao wafanye bidii
kuyatatua.
Naibu
Waziri Alhamisi aliendelea na ziara hiyo katika Halmashauri ya Wilaya
ya Mvomero na kukagua baadhi ya miradi ikiwemo Kibati, Kwadoli na
Kagugu. Vilevile, ametembelea bwawa la Mindu na kijijiji cha Lusungu.
Post a Comment