Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

NAIBU WAZIRI WA FEDHA ADAM MALIMA ASISITIZA UMUHIMU WA MASHINE ZA EFD KWA WAFANYABIASHARA NCHINI.

1Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima (kushoto) akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Mara John Tuppa (kulia) mara baada ya kuwasili katika ofisi za makao makuu ya mkoa wa Mara.2Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima akiongea na wa wafanyabiashara wa mkoa wa Mara juu ya umuhimu wa utumiaji wa mashine za kodi za kielektroniki (EFDs) kwa wafanyabiashara hao kukusanya kodi ya ongezeko la thamani (VAT) ili Serikali iweze kutoa mahitaji ya kijamii na uchumi kwa wakati.

3Kamishna wa Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Patrick Kasera akifafanua kwa wafanyabiashara wa mkoani Mara juu ya mashine za EFDs na kusema kuwa mashine hizo kazi yake kuu ni kutunza kumbukumbu za biashara hasa manunuzi na uuzaji na sio mfumo wa kodi kama ilivyopokelewa mwanzoni na wafanyabiashara nchini.4Baadhi ya wafanyabiashara wa mkoa wa Mara wakimsikiliza  Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima (hayupo pichani) alipokuwa alipozungumza na wafanyabiashara hao jana mjini Musoma katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa huo.
5Baadhi wa wajumbe waliohudhuria kikao cha wafanyabiashara wa mkoa wa Mara wakimsikiliza Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima alipozungumza nao ili kuwaelimisha juu ya masuala mbalimbali ikiwemo mashine za EFD wakati wa ziara yake ya kikazi mikoa ya kanda ya Ziwa.6Baadhi ya wafanyabiashara wa mkoa wa Mara wakimsikiliza  Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima alipokuwa alipozungumza na wafanyabiashara hao jana mjini Musoma katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa huo wakati wa ziara yake ya kikazi mikoa ya kanda ya Ziwa.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top