Shirikisho
la Soka la Kimataifa (Fifa), limetuma barua tatu tofauti kwa Mwenyekiti
wa Simba, Ismail Aden Rage, moja ikiwa ni ile inayomhusu Emmanuel Okwi
ambaye sasa yuko Yanga.
Moja
ya barua ambazo Rage amepewa kopi na Fifa ni ile ambayo Shirikisho la
Soka la Uganda (Fufa), limemuomba Okwi kurejea Uganda na kuitumikia timu
ya taifa katika michuano ya kimataifa.
Pamoja
na barua hiyo, Rage amethibitisha kupokea barua hizo tatu kutoka Fifa
ikiwemo ile ya Etoile du Sahel ya Tunisia kuomba kuongezewa muda wa
kulipa deni la dola 300,000 wanazodaiwa na Simba kutokana na mauzo ya
Okwi.
“Kweli
nimepokea barua hizo, moja ni ile ambayo Etoile ambao mwezi huu ndiyo
ulikuwa mwisho kulipa dola 300,000, sasa wameomba waongezewe muda hadi
Septemba, mwaka huu ili waweze kulipa.
“Fifa
wao wamenitumia kopi lakini barua hiyo ni kutoka kwao Etoile kwenda
Fifa na wamethibitisha kwamba ni kweli Simba inawadai,” alisema Rage.
Barua
ya tatu kati ya hizo kwa mujibu wa Rage ni ile ambayo inaonyesha namna
klabu hiyo ya Tunisia ilivyomshitaki Okwi kwa Fifa kutokana na kuonyesha
kukiuka mambo kadhaa wakati akijua mkataba wake nao unamalizika mwaka
2016.
“Katika
ile barua ya kuhusiana na suala la kulipa, Fifa wametaka tusaini na
kukubali kwamba sasa mwisho utakuwa Septemba 30 na tayari barua hiyo
nimeikabidhi kwa Hans Pope,” aliongeza Rage.
Tayari
Okwi yuko nchini na Yanga imemsajili ingawa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) limeamua kusimamisha usajili wake hadi litakapopata ufafanuzi
kuhusiana na usajili wake.
Wakati
Fifa ilitoa kibali kwa Okwi kucheza SC Villa ya Uganda kwa miezi sita,
lakini Yanga ikamnunua na kuingia naye mkataba wa miaka miwili, suala
ambalo limezua mzozo mkubwa huku Simba wakiendelea kusisitiza kulipwa
fedha zao ambazo mwanzo walimuuza na hawakulipwa.
Okwi
amekuwa akisisitiza kwamba anataka kuichezea Yanga ambayo imemsajili,
huku akieleza amekuwa akiumia moyoni kuona wenzake wakicheza naye akiwa
jukwaani kama mtazamaji.
SOURCE: CHAMPIONI
SOURCE: CHAMPIONI
Post a Comment