Waziri
wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa Na Serikali za Mitaa Hawa
Ghasia akieleza kwa waandishi wa Habari(Hawapo Pichani) kuhusu Mikakati
Madhubuti ya ukusanyaji mapato na Matumizi bora ya fedha zinazotolewa na
Serikali kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika Mikoa na Halmashauri
zote nchini, wakati wa Mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es
Salaam.Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah
Mwambene.
-Baadhi
ya waandishi wa Habari waliohudhuria Mkutano wa Waziri wa Nchi,Ofisi ya
Waziri Mkuu Tawala za Mikoa Na Serikali za Mitaa Hawa Ghasia, Katika
Ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam.Picha na Hassan Silayo.
MAELEZO
YA WAZIRI WA NCHI OWM-TAMISEMI KWA VYOMBO YA HABARI KUHUSU USIMAMIZI NA
UDHIBITI WA FEDHA KATIKA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA
1. UTANGULIZI
Usimamizi
wa fedha katika ngazi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa unaongozwa na
Sheria, Kanuni na Taratibu mbalimbali ambazo ni pamoja na:-
i. Sheria
ya Fedha ya Mamlaka za Serikali za Mitaa Sura ya 290 ambayo inaainisha
Mamlaka na taratibu mbalimbali zinazohusu Usimamizi wa fedha kwenye
Mamlaka za Serikali za Mitaa.
ii. Sheria ya Usimamizi wa Manunuzi ya Umma ya mwaka 2004 na kanuni zake za Mwaka 2005.
iii. Kanuni
za Usimamizi wa fedha katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ambazo ni
Mwongozo katika utaratibu na Usimamizi wa fedha kama ifuatavyo:-
– Memoranda
ya usimamizi wa fedha katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ya mwaka 1997
kama ilivyorekebishwa mwaka 2009 (Local Government Financial
Memorandum),
– Kanuni za Kudumu za Halmashauri,
– Kanuni za uanzishaji na uendeshaji wa Bodi za Zabuni katika Mamlaka za Serikali za Mitaa za mwaka 2007,
– Mwongozo wa uhasibu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa (Local Authority Accounting Manual) wa mwaka 2009,
– Mwongozo wa ukaguzi wa ndani wa mwaka 2005, na
– Mwongozo wa mipango na bajeti unaotolewa kila mwaka.
Usimamizi wa Sheria na Kanuni tajwa hapo juu ni nguzo muhimu katika kuimarisha utawala bora katika usimamizi wa fedha.Katika
masuala haya, Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI inasimamia kwa karibu
kuhakikisha Mamlaka za Serikali za Mitaa zinatekeleza majukumu yake
inavyopaswa.
Usimamizi wa fedha katika ngazi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa umegawanyika katika maeneo makuu yafuatayo:-
1. Vyanzo vya fedha (Financing Resources) - fedha za kuendeshea shughuli mbalimbali za Halmashauri;
2. Utumiaji wa fedha (Uses of Finance) - matumizi ya fedha zilizokusanywa na kupokelewa; na
3. Udhibiti
wa rasilimali (Controlling of Resources) - Namna ya kudhibiti
ubadhirifu au upotevu wa aina yeyote ile unaohusu rasilimali za Serikali
za Mitaa.
2. VYANZO VYA FEDHA ZA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA
Wajibu
wa msingi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa ni kutoa huduma za msingi za
kijamii na kusimamia Utawala Bora. Gharama za utoaji huduma hizo
unatokana na mapato ya kodi, ushuru na ada mbalimbali, ruzuku toka
Serikali Kuu, pamoja na misaada toka kwa Washirika wa Maendeleo na
Mikopo kutoka kwenye Taasisi mbalimbali za fedha. Hivyo vyanzo vya fedha
zaMamlaka za Serikali za Mitaa kisheria vimegawanyika katika makundi matatu yafuatayo:-
2.1 Mapato ya Ndani (Own Source Revenue).
Kwa
mujibu wa Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa Sura ya 290 Kifungu cha
6, 7, 8 na 9 vyanzo mbalimbali vya mapato vimeainishwa kwa Halmashauri
za Jiji, Miji, Wilaya na Vijiji. Vyanzo vilivyotajwa katika Vifungu
hivyo vinatoa nafasi kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa husika kutunga
Sheria Ndogo zitakazowezesha Mamlaka hizo kukusanya mapato kutokana na
vyanzo hivyo. Miongoni mwa mapato hayo ni ushuru wa leseni, ushuru wa
kodi ya huduma, ushuru wa mazao, Kodi ya majengo, ushuru wa magulio na
masoko na ada za kuegesha magari.
Mapato
ya Halmashauri kutoka vyanzo vyake vya ndani kwa miaka nane (2005
-2013) iliyopita yanaonesha kuwa makisio na makusanyo ya mapato ya
Mamlaka za Serikali za Mitaa yamekuwa yanaongezeka. Mfano, kwa miaka
mitano iliyopita yaani Mwaka 2008/09 makisio yalikuwa ni shilingi bilioni 107.6na makusanyo halisi yalikuwa shilingi bilioni 93.7 ambayo niasilimia 87 ya makadirio. Kwa mwaka wa fedha 2009/10 makadirio yalikuwa shilingi bilioni 130.9 ambapo makusanyo yalikuwa shilingi bilioni 117.8 sawa na asilimia 90 ya
makadirio. Mapato haya yameendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka ambapo
kufikia Mwaka 2012/13 makadirio yalikuwa kukusanya shilingi bilioni 328.4 na makusanyo yalikuwa shilingi bilioni 240.9sawa na asilimia 73.3. Ongezeko la makadirio kwa miaka hii nane yaani kutoka 2005/06 hadi 2012/13 ni sawa na asilimia 512.9wakati makusanyo yameongezeka kwa asilimia 389. Mtiririko wa mapato hayo kwa kipindi hicho ni kama inavyoonekana katika jedwali lifuatalo:
Mwenendo Wa Mapato ya Ndani ya Halmashauri kuanzia Mwaka 2005/6 Hadi Mwaka 2012/13
| |||
Mwaka
|
Makadirio
|
Makusanyo Halisi
|
% Ya Makusanyo
|
2005/06
|
53,593,591,293
|
49,291,049,660
|
92.0
|
2006/07
|
63,385,237,737
|
61,411,259,961
|
96.9
|
2007/08
|
80,136,598,991
|
79,770,210,999
|
99.5
|
2008/09
|
107,628,203,817
|
93,752,903,592
|
87.1
|
2009/10
|
130,887,328,313
|
117,783,506,345
|
90.0
|
2010/11
|
175,084,789,727
|
158,279,374,601
|
90.4
|
2011/12
|
310,962,562,609
|
195,524,503,634
|
62.9
|
2012/13
|
328,450,131,918
|
240,908,504,656
|
73.3
|
Mwenendo
wa ukusanyaji wa mapato unaonesha kuwa Mamlaka za Serikali za Mitaa
zimeendelea kujitahidi katika ukusanyaji. Hata hivyo Serikali inaendelea
kuzijengea uwezo Halmashauri ili ziweze kufikia malengo ya ukusanyaji
waliojiwekea. Kwa sasa Serikali kwa kushirikiana na Washirika wa
Maendeleo imeendelea kufanya yafuatayo:-
· OWM
– TAMISEMI imekamilisha utafiti wa vyanzo vya mapato katika Mamlaka za
Serikali za Mitaa 30 (za majaribio) katika kipindi cha Julai – Septemba,
2013, ambapo vyanzo mbalimbali vipya vinavyoweza kutozwa Kodi
vimeibuliwa kama Kodi ya majengo kwa Halmashauri za Wilaya, Ushuru wa
Mifugo, Ushuru wa Minara ya Simu, Ushuru wa nyumba za kulala wageni
uliofutwa awali nk. Maeneo hayo yatapanua wigo wa mapato wa Halmashauri
pamoja na maeneo yanayotakiwa kufanyiwa marekebisho ya Kisheria (Sheria
ya Fedha za Mamlaka za Serikali za Mitaa ya mwaka 1982) ili kuongeza
wigo wa mapato. Vile vile, utafiti huo umeangalia njia za kuongeza
ufanisi katika ukusanyaji wa mapato pamoja na njia za malipo rahisi ili
kupunguza kero na umbali kwa walipaji hasa katika kulipa kupitia
teknolojia rahisi za malipo kwa kutumia M- Pesa, Tigo – Pesa, Max-
Malipo, n.k.
· OWM-TAMISEMI
kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara imerudisha Ada za
Leseni za Biashara kuanzia mwezi Julai, 2013 ili kuziwezesha Mamlaka za
Serikali za Mitaa kuongeza vyanzo vya ukusanyaji wa mapato.
· OWM-TAMISEMI
itaendelea kusimamia kikamilifu Mamlaka za Serikali za Mitaa katika
kuhakikisha zinakusanya mapato yake ya ndani ipasavyo ikiwa ni pamoja na
kutumia mifumo ya kielektroniki ya usimamizi wa mapato yaani “Local
Government Revenue Collection System (LGRCS)” na “i-TAX”kwa lengo la
kuboresha usimamizi na udhibiti wa mapato ya ndani ya Halmashauri na
kuhakikisha mapato haya yanatumika inavyopaswa.
· Halmashauri
zimeendelea kuchukua hatua za Kisheria kwa Mawakala wote ambao
hawajawasilisha makusanyo ya mapato pamoja na wale wote wanaokwepa
kulipa ushuru kulingana na taratibu zilizopo. Mfano mwaka 2011/12
Mawakala 35 wa ukusanyaji mapato katika Halmashauri mbalimbali
wamefikishwa Mahakamani kwa kutowasilisha makusanyo kulingana na
makubaliano.
· OWM-TAMISEMI
imeendelea kuzielekeza Halmashauri zote nchini kubuni vyanzo vipya vya
mapato kulingana na uwezo na uchumi wa maeneo yao ili kuwaongezea
kipato. Kadhalika, maelekezo yametolewa kwa Halmashauri kuhakikisha kodi
zinazotozwa sasa zinakusanywa kikamilifu na kwamba mbinu za ukusanyaji
zinaboreshwa ili kuongeza mapato. Mikoa nayo imeagizwa kutekeleza jukumu
lake la msingi la kuzisaidia na kusimamia Halmashauri ipasavyo ikiwemo
eneo la ubunifu wa vyanzo vya mapato.
2.2 Ruzuku toka Serikalini na kwa Washirika wa Maendeleo
Mamlaka
za Serikali za Mitaa kwa mujibu wa Kifungu cha 10 cha Sheria ya Fedha
za Mamlaka za Serikali za Mitaa zinapaswa kupokea ruzuku toka Serikali
Kuu ili kulipia gharama za utoaji wa huduma mbalimbali kama Afya, Elimu,
Kilimo, Barabara na maji. Ruzuku hii ni kwa ajili ya Matumizi ya
Kawaida, Mishahara na Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo. Suala
la kupeleka fedha za ruzuku katika MSM linategemea upatikanaji wa fedha
za makusanyo ya ndani ya Serikali na kutoka kwa Washirika wa Maendeleo.
Pale ambapo Serikali Kuu imekusanya mapato kidogo kutoka katika vyanzo
hivyo, upelekaji wa fedha katika MSM nao huwa mdogo.
2.3 Mikopo ya Mamlaka za Serikali za Mitaa
Mamlaka
za Serikali za Mitaa kwa mujibu wa Kifungu cha 11 cha Sheria ya Fedha
za Mamlaka za Serikali za Mitaa Sura 290 zina fursa ya kukopa kutoka
katika Taasisi za fedha na Mabenki ili kupata fedha kwa ajili ya
utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Hadi kufikia Juni, 2013 Halmashauri
zipatazo 21 zimepatiwa Mikopo kupitia Taasisi za binafsi za Fedha. Pia
Kifungu na 12 cha Sheria hiyo kinatoa nafasi kwa Halmashauri kutumia
fedha zaidi ya akiba iliyopo Benki kwa kupata kibali cha Waziri mwenye
Dhamana ya Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Kadhalika,
Mamlaka za Serikali za Mitaa zinaruhusiwa kukopa fedha kutoka Bodi ya
Mikopo ya Serikali za Mitaa. Hadi kufikia Septemba, 2013 Bodi ya Mikopo
ya Serikali za Mitaa imeweza kutoa mikopo ya jumla ya Shs.
6,935,736,734/=. Aidha, zipo Halmashauri zilizowasilisha maombi ya
mikopo ambayo yanaendelea kushughulikiwa ili yaweze kupata vibali vya
kukopa. OWM – TAMISEMI imendaa Mwongozo maalum unaozielekeza Mamlaka za
Serikali za Mitaa kuzingatia taratibu muhimu za kufuatwa kabla ya
kuwasilisha maombi ya Vibali vya mikopo.
3. UTUMIAJI WA FEDHA
Usimamizi
katika matumizi ya fedha za Umma unaanzia katika utengenezaji wa
bajeti. Serikali huandaa Mwongozo wa namna ya kuandaa bajeti kila mwaka
ambapo Mamlaka za Serikali za Mitaa huutumia kuandaa bajeti zao kwa
kuzingatia ushirikishwaji wa jamii katika kuibua Miradi ya Maendeleo
kulingana na mahitaji ya eneo husika. Katika Usimamizi wa Mapato na
Matumizi ya Fedha za Mamlaka za Serikali za Mitaa, Kanuni
za Usimamizi wa Fedha wa Mamlaka za Serikali za Mitaa (LAFM, 2009)
zimeainisha wajibu na majukumu ya makundi mbalimbali ya Viongozi na
Watendaji katika Mamlaka hizo ambao wana wajibu wa kusimamia matumizi
hayo kama ifuatavyo:
3.1 Waziri mwenye Dhamana ya Mamlaka za Serikali za Mitaa
Kuhakisha
kuwa upo usimamizi madhubuti wa mapato na matumizi katika Mamlaka za
Serikali za Mitaa; kuwezesha kuwepo kwa usalama wa fedha kwa ajili ya
shughuli za Mamlaka za Serikali za Mitaa na kuhakikisha kuwa Mamlaka za
Serikali za Mitaa zinatekeleza shughuli zake kwa mujibu wa mipango na
bajeti ikiwemo kuziwezesha
ili ziweze kutoa huduma bora kwa wananchi. Kadhalika kuchukua hatua
stahiki kwa Watendaji watakaobainika kufanya ubadhirifu wa mali ya umma.
3.2 Mkuu wa Mkoa.
Kuhakiki
na kupitia taarifa za mapato na matumizi ikiwemo zile za utekelezaji wa
miradi ya maendeleo za kila robo mwaka; kutoa ushauri katika mipango na
bajeti za Halmashauri; kupitia taarifa za Mkaguzi wa Ndani za kila robo
mwaka; kupitia taarifa za Kamati za Ukaguzi (Audit Committee), kufanya
ukaguzi maalum wa masuala ya fedha na kuchukua hatua stahiki kulingana
na Sheria, Taratibu na Kanuni zilizopo.
3.3 Baraza la Madiwani.
Baraza
la Madiwani lina wajibu wa kutoa maamuzi katika masuala yote ya
usimamizi wa utekelezaji wa shughuli za Mamlaka za Serikali za Mitaa
ikiwemo kuidhinisha mipango na bajeti za Halmashauri; kujadiliana,
kukubali au kukataa mapendekezo ya taarifa za utekelezaji
zilizowasilishwa na Kamati za Kudumu pamoja na kuchukua hatua stahiki
kwa watumishi walioenda kinyume na Sheria.
3.4 Kamati ya Fedha na Uongozi.
Kudhibiti
na Kusimamia Mapato na Matumizi ya Halmashauri kwa kupitia taarifa za
mapato na matumizi ya kila mwezi; taarifa za utekelezaji wa Miradi ya
Maendeleo ya kila robo mwaka; taarifa za Mkaguzi wa ndani na zile za
Kamati ya Ukaguzi. Pia kuidhinisha mipango na bajeti ya mwaka ya
Halmashauri; kupitia taarifa za Bodi ya Zabuni; kupitia taarifa za
Kitengo cha Manunuzi cha Halmashauri (PMU), na kusimamia uwasilishaji
wa taarifa za mwisho wa mwaka wa fedha kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali.
3.5 Menejimenti ya Halmashauri.
Mkurugenzi
ndiye Afisa Masuuli wa Halmashauri kwa hiyo kwa kushirikiana na Wakuu
wa Idara, anao wajibu wa kuhakikisha kuwa Halmashauri ina mfumo rasmi na
wa kuridhisha wa usimamizi wa fedha; Sheria, Kanuni na Miongozo ya
Usimamizi wa fedha inafuatwa kwa ukamilifu na Idara zote katika
utekelezaji wa shughuli za Halmashauri; kusimamia Mapato, Matumizi, Mali
na Madeni yote ya Halmashauri; kujibu Hoja za ukaguzi za Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Mkaguzi wa Ndani na Kamati zozote za
Ukaguzi kwa wakati na ukamilifu; pamoja na kuhakikisha kuwa Madiwani
wanapewa taarifa zinazohusu masuala ya fedha kwa wakati.
Katika
kutekeleza majukumu haya ya usimamizi kwa upande wa matumizi, zipo
taarifa mbalimbali zinazoandaliwa katika ngazi zote zinazoonesha mapato
yaliyopatikana na namna fedha hizo zilivyotumika. Lengo ni kuona fedha
hizi zimetumika katika maeneo yaliyokusudiwa na kwamba thamani ya fedha
hizo inaonekana ili hatimaye kutoa huduma za msingi kwa wananchi.
Taarifa hizi huonesha mapato na matumizi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa ikiwemo miradi ya maendeleo na hupitiwa na Vikao na Kamati mbalimbali zikiwemo; Baraza la Madiwani, Kamati ya Huduma za Jamii, Kamati ya Huduma za Kiuchumi na Kamati ya Fedha na Uongozi/Mipango).
Kamati
ya Fedha na Uongozi inakutana kila mwezi. Baraza la Madiwani na Kamati
za Huduma za Jamii na Huduma za Kiuchumi hukutana angalau mara moja kila
robo mwaka. Kamati hizi hujadili na kujiridhisha kama taarifa hizi ni
sahihi na kama zinawakilisha matakwa ya wananchi kwa mujibu wa mipango
na bajeti za kila mwaka. Matakwa ya wananchi yanapatikana kwa
kuwahusisha na kuwashirikisha katika Vikao vya kupanga na kuamua
vipaumbele vinavyotokana na mazingira, nyakati na mahitaji waliyonayo.
Taarifa
hizi hupelekwa ngazi ya Mkoa ambapo huthibitishwa usahihi wake,
kuunganishwa na kuwasilishwa OWM-TAMISEMI kwa uchambuzi na kutoa maamuzi
mbalimbali.
4. UDHIBITI WA RASILIMALI
Serikali
inawajibika kwa wananchi ambao ni walipa kodi na Washiriki wa Maendeleo
wanaotupatia misaada kuhakikisha kuwa fedha zao zinatumika kwa
maendeleo ya nchi na hazifujwi.
4.1 Mfumo wa Usimamizi wa Fedha (Epicor 9.05)
Ili
kuhakikisha kunakuwepo matumizi sahihi ya fedha na utoaji taarifa,
Serikali ilianzisha mfumo wa kudhibiti matumizi ya fedha yaani
“Intergrated Financial Management System (IFMS)”. Katika Serikali kuu
maboresho haya yalianza na Wizara 5 za Kisekta na upande wa Serikali za
Mitaa mfumo huu ulifanyiwa majaribio kwenye Halmashauri 38 mwaka
1999-2002. Mfumo wa IFMs (Epicor 9.05) ulioanzishwa unasaidia utunzaji
wa kumbukumbu za kihasibu na usimamizi wa fedha ikiwa ni pamoja na
utumiaji wa mfumo katika kutunza hesabu za Halmashauri. Hadi sasa Mikoa
21 na Halmashauri 133 zimeunganishwa kwenye mfumo huu na mpango wa
Serikali hadi kufikia mwaka wa fedha 2014/2015 ni kuunganisha pia Mikoa
na Halmashauri mpya zote zilizoanzishwa.
Mfumo
huu wa usimamizi wa fedha upo ili kudhibiti upotevu na matumizi mabaya
na pia unauhakikishia umma kwamba kuna matumizi mazuri ya fedha na
rasilimali nyingine, uwajibikaji, uwazi, na kwamba matumizi ya fedha
hizo yanaonesha thamani halisi ya fedha zilizotumika (value for money).
4.2 Vyombo vingine vya udhibiti
Pamoja
na kuwepo kwa maelezo ya wazi kuhusu wajibu na majukumu ya kila
Kiongozi na Mtendaji, Sheria, Kanuni na Taratibu za usimamizi wa fedha
za Mamlaka za Serikali za Mitaa zimeainisha mfumo na vyombo
vinavyoangalia utekelezaji wa shughuli za Halmashauri zilizopangwa
ikiwemo kuhakikisha miongozo bora ya Uhasibu na utunzaji fedha inazingatiwa. Vyombo hivyo ni pamoja na:-
a. Mkaguzi wa Ndani
Halmashauri
zinapaswa kuwa na Mkaguzi wa Ndani kwa mujibu wa Kifungu cha 45 cha
Sheria za Mamlaka za Serikali za Mitaa. Wajibu wake ni kukagua na
kutathmini umadhubuti na ukamilifu wa Mfumo wa Udhibiti wa ndani ambao
umewekwa kuhakikisha malengo ya Taasisi yanafikiwa. Serikali imeendelea
kuboresha Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani cha Halmashauri kwa kuwapatia
vitendea kazi na mafunzo mbalimbali ili kuwajengea uwezo katika
kuhakikisha udhibiti wa rasilimali za Halmashauri unaimarika.
b. Kamati ya Ukaguzi ya Halmashauri
Kamati ina wajumbe wa ndani na nje ya Halmashauri. Wajibu wake ni kutathmini mpango kazi na taarifa za Mkaguzi wa Ndani, kuhakikisha
taarifa za Mapato na Matumizi ni sahihi, za kuaminika na kamilifu
(accurate, reliable and complete), hivyo kupunguza/kuondoa uwezekano wa
kupata hati chafu za Ukaguzi kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali. Kadhalika kutoa
maoni na ushauri kwa Afisa Masuuli kuhusu masuala yanayohusu hoja
mbalimbali za ukaguzi na udhaifu wa usimamizi wa fedha ili kurekebisha
kasoro zilizobainika na hatimaye kuwezesha rasilimali kutumika kwa uadilifu na kwa madhumuni yaliyokusudiwa.
c. Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC)
Kamati
hii ina wajibu wa kupitia taarifa za fedha zinazowasilishwa na
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali za kila mwaka pamoja na
majibu ya hoja hizo; kuchambua na kuhakiki taarifa za mapato, matumizi
na utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Mamlaka za Serikali za
Mitaa pamoja na kuhakiki miradi ya maendeleo na matumizi ya mifuko ya
pamoja. Katika kutekeleza majukumu hayo, Kamati hufanya Vikao ambapo
Halmashauri hutakiwa kuwasilisha taarifa zao za mapato na matumizi na
kisha kujadiliwa na kupewa maelekezo au mapendekezo ya namna ya
kuboresha utendaji wa kazi. Aidha Kamati pia hutembelea na kukagua
miradi ya maendeleo kulingana na mipango ya Halmashauri ili kuona kama
thamani ya fedha imepatikana na huduma hizo zinakidhi mahitaji ya
wananchi.
OWM
– TAMISEMI inaendelea kushirikiana na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya
Hesabu za Serikali za Mitaa ili kuhakikisha kuwa Sheria, Kanuni na
Taratibu za Fedha za Serikali za Mitaa zinafuatwa na kila mhusika,
pamoja na kuona kuwa Halmashauri zinajirekebisha na kuendelea kupata
Hati Safi. Vilevile Ofisi hii pia imeendelea kuhakikisha kuwa
inawachukulia hatua za kinidhamu Watendaji ambao siyo waadilifu katika
masuala ya fedha kwa mujibu wa Sheria.
d. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mujibu wa Kifungu namba 48
cha Sheria ya Fedha ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa amepewa Mamlaka ya
kukagua rasilimali, mifumo ya uendeshaji, utekelezaji wa shughuli za
Miradi ya Maendeleo ya Mamlaka za Serikali za Mitaa, na kwa mujibu wa
Sheria ya Ukaguzi namba 19/2008 anapaswa kukagua na kutoa taarifa yenye
hati za maoni kuhusu taarifa za fedha jinsi zinavyoonesha utekelezaji wa
shughuli za Mamlaka za Serikali za Mitaa kila mwaka pamoja na Kufanya ukaguzi maalum pale inapobidi.
Kiuhalisia
Halmashauri zimeendelea kufunga vitabu na kuwasilisha hesabu hizo kwa
Wakaguzi kwa wakati. Kwa mujibu wa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za Serikali, hali ya usimamizi na utunzaji wa vitabu vya
hesabu za fedha kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa imeendelea
kuimarika. Mtiririko wa Hati kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa unaonesha
kuwa hati zisizoridhisha zimeendelea kupungua, mfano mwaka 2011/12
hakuna Halmashauri iliyopata Hati isiyoridhisha ikilinganishwa na
Halmashauri nne za mwaka 2005/06. Kadhalika kwa miaka nane iliyopita
hati safi zimeendelea kuongezeka ambapo mwaka 2011/12 Halmashauri 104
sawa na asilimia 78 zilipata Hati Safi ikiwa ni ongezeko la Halmashauri
51 kutoka Halmashauri 53 za mwaka 2005/06.
Mwenendo
wa matokeo ya Ukaguzi wa Hesabu za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa
miaka nane (8) ni kama inavyoonekana katika jedwali linalofuata.
Mwaka
|
Hati Safi
|
Asilimia
|
Hati Yenye shaka
|
Asilimia
|
Hati Chafu
|
Asilimia
|
Hakuna maoni (Disclaimer
|
Asilimia
|
Jumla
|
2004/5
|
62
|
53%
|
51
|
44%
|
4
|
3%
|
-
|
-
|
117
|
2005/6
|
53
|
43%
|
67
|
54%
|
4
|
3%
|
-
|
-
|
124
|
2006/7
|
100
|
81%
|
24
|
19%
|
-
|
-
|
-
|
-
|
124
|
2007/8
|
72
|
54%
|
61
|
46%
|
-
|
-
|
-
|
-
|
133
|
2008/9
|
77
|
58%
|
55
|
41%
|
1
|
1%
|
-
|
-
|
133
|
2009/10
|
66
|
49%
|
64
|
48%
|
4
|
3%
|
-
|
-
|
134
|
2010/11
|
72
|
54%
|
56
|
42%
|
5
|
4%
|
-
|
-
|
133
|
2011/12
|
104
|
78%
|
29
|
21%
|
-
|
-
|
1
|
1
|
134
|
Ni
mategemeo ya Serikali kuwa Halmashauri nyingi zaidi zitaendelea kupata
hati safi kutokana na jitihada mbalimbali za udhibiti na usimamizi wa
fedha zinazoendelea ikiwemo matumizi ya mfumo wa IFMS-Epicor 9.05,
pamoja na uimarishwaji wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani wa Halmashauri
pamoja na Ofisi za Mikoa zinazosimamia utekelezaji wa shughuli za
Halmashauri kwa karibu zaidi.
HATUA ZA KINIDHAMU ZILIZOCHUKULIWA KWA WATENDAJI
Pamoja
na kuimarika kwa usimamizi wa rasilimali za MSM, kumekuwepo na vitendo
vya baadhi ya Watendaji katika ngazi hizo kufuja mali za umma kinyume na
taratibu zilizopo. Hata hivyo Serikali imeendelea kuwachukulia
Watumishi hao hatua za Kinidhamu na Kisheria kulingana na makosa
waliyofanya. Hatua hizi ni pamoja na kufukuzwa kazi, kupewa onyo,
kuvuliwa madaraka, kushushwa mshahara, kufikishwa Mahakamani pamoja na
kutakiwa kurejesha fedha zilizopotea. Hatua hizo zimekuwa zikichukuliwa
pale inapobainika au kuthibitika Watumishi wameshindwa kutekeleza wajibu
wao. Hadi kufikia mwezi Septemba, 2013 hatua za Kinidhamu/Kisheria
zimechukuliwa kwa Watumishi mbalimbali waliofanya ubadhirifu kama
inavyoonesha katika mchanganuo hapa chini:-
Jumla
ya Wakurugenzi 53, Wakuu wa Idara 65 na Watumishi wengine 749 katika
Mamlaka za Serikali za Mitaa wamechukuliwa hatua mbalimbali za kinidhamu
kufuatia kuhusishwa na ubadhirifu wa fedha za umma kama ifuatavyo:-
1. Wakurugenzi;
(i) Waliofukuzwa Kazi ni mmoja (1),
(ii) Waliosimamishwa kazi ni sita (6),
(iii) Waliovuliwa Madaraka ni ishirini na tano (25),
(iv) Waliopewa ONYO ni kumi na mbili (12),
(v) Waliofikishwa Mahakamani ni nane (8) na
(vi) Walioshushwa mshahara ni mmoja (1).
2. Wakuu wa Idara;
(i) Waliofukuzwa kazi ni 14,
(ii) Waliosimamishwa kazi ni 12,
(iii) Waliopewa ONYO ni 16,
(iv) Waliovuliwa madaraka ni tisa (9),
(v) Waliofikishwa Mahakamani ni 13 na
(vi) Waliofikishwa Polisi na TAKUKURU ni mmoja (1).
3. Watumishi wengine;
(i) Waliofukuzwa kazi ni 217,
(ii) Waliosimamishwa kazi ni 168,
(iii) Walioshushwa cheo ni wanne (4),
(iv) Walioshushwa cheo ni 28,
(v) Waliopewa ONYO ni 85,
(vi) Waliofikishwa Mahakamani ni 212 na
(vii) Waliofikishwa Polisi na TAKUKURU ni 35.
CHANGAMOTO ZINAZOZIKABILI MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA
Pamoja
na jitihada za Serikali za kuhakikisha MSM zinawezeshwa ili kutoa
huduma bora kwa wananchi bado, zipo changamoto mbalimbali ambazo
zinaendelea kupatiwa ufumbuzi. Miongoni mwao ni pamoja na:-
1. Utegemezi
mkubwa wa fedha za Ruzuku kutoka Serikali Kuu ili kutekeleza shughuli
za maendeleo. Mapato ya ndani ya Halmashauri yanayokusanywa hayatoshi
kukidhi mahitaji ya wananchi hivyo kuzifanya Mamlaka za Serikali za Mitaakutegemea
Ruzuku na Misaada ya Washiriki wa Maendeleo. Hata hivyo, Halmashauri
zimeendelea kuhimizwa kubuni vyanzo vipya vya mapato na kuhakikisha vile
vilivyopo vinakusanywa kwa ukamilifu.
2. Baadhi ya watumishi kutokuwa waaminifu na kuendelea kutumia fedha za umma isivyo halali.
3. Uhaba wa watumishi na vitendea kazi.
4. Baadhi ya wadau mbalimbali kutokukubali Mfumo wa usimamizi wa fedha ulioanzishwa wa IFMS – Epicor 9.05.
MIKAKATI ILIYOWEKWA KUONGEZA UWAJIBIKAJI NA NIDHAMU KATIKA MATUMIZI NA KUDHIBITI UBADHIRIFU WA MALI/FEDHA ZA UMMA
Mikakati iliyowekwa na Serikali ili kuongeza uwajibikaji na udhibiti wa mali za Umma ni kama ifuatavyo:-
1. Kutoa
maelekezo kwa Halmashauri zote nchini kufanya ukaguzi wa mara kwa mara
hususan katika miradi ya maendeleo kwa kutumia vyombo vifuatavyo:-
a. Timu ya Menejimenti ya Halmashauri (CMT),
b. Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango,
c. Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani,
d. Kamati ya Ukaguzi ya Halmashauri, na
e. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
2. Kuendelea
kuzijengea uwezo Sekretarieti za Mikoa ili ziweze kushauri na kusimamia
utekelezaji wa shughuli za Halmashauri ikiwemo ukaguzi wa miradi ya
maendeleo na kuchukua hatua stahiki wa watumishi watakaobainika kufanya
ubadhirifu.
3. Kuendelea
kuimarisha Kitengo cha Ukaguzi wa Awali na Kitengo cha Ukaguzi wa
Ndani wa Halmashauri kwa kuwapatia Wakaguzi wa ndani vitendea kazi ili
kurahisisha ufuatiliaji katika maeneo yao, sambamba na kuendelea kufanya
mafunzo kwa Wakaguzi wote wa Ndani wa Halmashauri na wale walio
Mkoani.
4. Viongozi
wa OWM-TAMISEMI pamoja na Wataalam kuendelea kufuatilia na kufanya
ukaguzi kwa Mikoa na Halmashauri kwa lengo la kuangalia uendeshaji wa
shughuli za Halmashauri ikiwa ni pamoja na Miradi ya Maendeleo.Pia kupeleka nyenzo kama magari, pikipiki na Kompyuta.
5. Kuendelea
kuimarisha mifumo ya uhasibu na udhibiti wa ndani kupitia Mfumo wa
usimamizi wa fedha wa IFMS- EPICOR 9.05 kwa upande wa “technical“ na
“application“ ili kuhakikisha nidhamu ya bajeti na taratibu za matumizi
ya fedha vinafuatwa. Hii itahusisha marekebisho katika Mtandao wa
mawasiliano hususan Halmashauri za pembezoni pamoja na kukamilisha
“module” mbalimbali zitakazotumika katika uaandaji wa taarifa za fedha
na ufungaji wa Hesabu. Mfumo pia utaendelea kutumika kufuatilia kwa
karibu na kudhibiti matumizi yanayofanywa na Halmashauri moja kwa moja
kulingana na Sheria za Fedha.
6. Kufunga
Mfumo wa IFMS-EPICOR 9.05 katika Halmashauri na Mikoa mipya
iliyoanzishwa pamoja na kutoa mafunzo kwa Waweka Hazina na Wahasibu wa
Halmashauri JUU ya namna ya kuutumia ipasavyo.
7. Kuendelea
kutoa miongozo mbalimbali kwa Mikoa na Halmashauri juu ya matumizi
sahihi ya fedha za Umma pamoja na kuendelea kuchukua hatua za kinidhamu
kwa watumishi wanaobainika kufanya ubadhirifu wa mali ya Umma kulingana
na Sheria zilizopo.
8. Kuendelea
kutoa mafunzo kwa watendaji wa Halmashauri na Mikoa juu ya usimamizi wa
fedha, manunuzi, ukaguzi na majukumu yao kwa wananchi pamoja na
uwajibikaji.
Post a Comment