Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma(PPRA) imebaini ufisafi wa
Sh13.48 bilioni katika miradi miwili ya ujenzi wa majengo ya Mfuko wa
Akiba ya Wafanyakazi(GEPF) na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini
(Rita) baada ya kufanya ukaguzi katika majengo hayo.
Kadhalika PPRA, imeagiza GEPF kurejesha kiasi cha
Sh847 milioni kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutokana na
udanganyifu kwa kuagiza vifaa kupitia msamaha wa kodi uliotolewa, ambapo
vifaa hivyo havikutumika katika mradi huo kwa mujibu wa maelewano.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari jana Dar es
Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA, Matern Lumbanga alisema timu ya
wataalamu iliyoundwa kufanya uhakiki kuhusu hoja zilizotolewa awali
ambazo zilionyesha malipo yenye shaka yaliyofanywa na taasisi hizo.
Lumbanga alisema, timu ya wataalamu ilibaini kuwa
malipo yenye shaka kwa mkandarasi wa mradi wa GEPF yenye thamani ya
Sh8.43 bilion ambayo ni sawa na asilimia 93 ya malipo yote yaliyobainika
awali kuwa na utata.
Awali, ukaguzi wa PPRA uligundua malipo yenye
shaka ya Sh7.37 bilioni, ambayo yalilipwa kinyume na mkataba. Pia
mamlaka iligundua kuwapo kwa malipo ya Sh2.31 bilioni yaliyofanyika nje
ya mkataba.
Hata hivyo, alisema GEPF na Rita walipingana na hoja za ukaguzi na hivyo PPRA ilimowaomba mtaalamu mshauri kuhakiki ukaguzi huo
“Mshauri alikuta malipo ya shaka kwa GEPF
waliongezeka kwa Sh1.6 bilioni na kufanya malipo yenye shaka ya Sh9.01
bilioni, na kwa upande wa Rita malipo waliongezeka kwa Sh5.3 6 bilioni
na kufanya malipo shaka kuwa Sh7.67 bilioni,” alisema Lumbanga.
Alisema, GEPF walikubali hoja za ukaguzi kwa kiasi
cha Sh3.23 bilioni sawa na asilimia 36 ya malipo yaliyoonekana kuwa na
shaka , wakati Rita walikubali kwa asilimia 49 ya thamani ya hoja za
ukaguzi zilizothibitishwa na mtaalamu huyo.
Kutokana na kutoridhishwa kwa wadaiwa hao, GEPF na
Rita, ndipo PPRA iliunda timu ya wataalamu kutoka Kamati ya Wataalamu
wa Bodi ya Wakurugenzi wa PPRA, Baraza la Taifa la Ujeni (NCC), Bodi ya
Usajili ya Wabunifu Majengo, Wakadiriaji Majenzi(AQRB) na wataalamu
washauri wa PPRA.
Utafiti huo uligundua malipo yenye shaka ya Sh
8.43 bilioni ambayo ni sawa na asilimia 93.5 ya malipo yote ya
liyobainika kuwa na utata na ukaguzi katika mradi wa GEPF, huku malipo
shaka katika mradi wa RITA yakiwa Sh5.05 bilioni. Kutokana na matokeo ya
timu ya wataalamu PPRA, imeagiza GEPF kurejesha pesa kiasi cha Sh 847
bilioni kwa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) baada ya kufanya udanganyifu
katika ununuzi wa vifaa vya ujenzi wa jengo hilo.
Pia imeagiza GEPF kukata malipo ya mkandarasi
kiasi cha Sh1.5 bilioni kama fidia baada ya kuchelewesha ukamilishaji wa
mradi kwa siku 127 tofauti na muda ulipangwa awali yaani kutoka Juni 30
hadi Novemba mwaka 2013, na pia mradi huo utaendelea kukata kiasi cha
Sh47 bilioni kutoka katika salio la malipo ya mkandarasi kutokana an
marekebisho yaliyofanyika kwenye msingi.
MWANANCHI
MWANANCHI
Post a Comment