MWANAUME
mmoja alichomwa kisu hadi kufa wakati akitazama mechi ya kandanda
mjini Meru baada ya kutofautiana na mwenzake kuhusu mechi iliyokuwa
ikiendelea.
Marehemu
alikuwa akitazama mchuano kati ya timu ya Arsenal na Liverpool wakati
walipoanza vita katika baa ya Marete eneo la Makutano.
Akithibitisha
kisa hicho, Mkuu wa Polisi eneo hilo Tom Odero alisema mshukiwa David
Mwangi, ambaye ni shabiki wa timu ya Arsenal alimdunga kisu Anthony
Muteithia, shabiki wa Liverpool. Bw Odero alisema mwanaume huyo mwenye
umri wa miaka 25 alikufa alipokuwa akipata matibabu katika Hospitali ya
Wilaya ya Meru.
“Mshukiwa
alilazimika kutoroka lakini wakazi walifanikiwa kupata pikipiki
aliyokuwa nayo na kuiwasilisha kwa maafisa wa polisi katika kituo cha
polisi cha Meru. Msako wa kumkamata umeanzishwa,”alisema Bw Odero.
Mkuu huyo wa polisi alisema uchunguzi umeanzishwa kutambua chanzo cha mzozo wa wawili hao.
Katika mchezo huo Arsenal walichapwa 5-1 na Liverpool.
Post a Comment