Baadhi ya Maboksi ya Vitabu yaliyokabidhiwa kwa shule 22 zilizoko wilaya ya kilolo.
======== ======= =========
Na Denis Mlowe,Ilula
Katika
kuhakikisha kiwango cha elimu nchini kinakua,shirika lisilo la
Kiserikali la Campaign for Female Education (CAMFED) chini ya mpango
wake kuwasomesha watoto wa kike limetoa misaada ya vitabu 54,935 kwa
shule 22 za sekondari zilizoko katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa
vyenye thamani ya shilingi milioni 55.
Akiongea
wakati wa halfa ya kukabidhi vitabu iliyofanyika katika Shule ya
Sekondari Ilula mwishoni mwa wiki mgeni rasmi Mwenyekiti Huduma za Jamii
wa Halmashauri ya wilaya Kilolo, Anna Kulanga alilishukuru shirika hilo
kwa msaada huo kwa kuweza kuwafikia wanafunzi wa shule za Iringa
vijijini.
“Tumefurahi
sana kupata vitabu mbalimbali kwani shule ya sekondari za hapa
zina changamoto ya upungufu wa vitabu hasa vya sayansi na kulifanya
somo hilo kuwa na wanafunzi wa chache, lakini hivi sasa kutokana na
msaada wa vitabu vilivyo tolewa vitaongeza ufaulu kwa wanafunzi wetu
kutokana na uwingi wa vitabu wenyewe kwa shule zilizofaidika na msaada
huo” alisema Kulanga
Aliwataka
walimu na wanafunzi wavitumie vitabu hivi vizuri kwa kuvitunza kwa
lengo la kutumika kwa muda mrefu wakati wa masomo yao na kuamini kwamba
vitabu vivyo vitaleta ufanisi katika kukuza uelewa wa mwanafunzi katika
matumizi sahihi ya lugha ya kiingereza.
Aidha
alisema vitabu hivyo vitumike kwa wanafunzi wote kwa wa shule husika na
kuwaasa wanafunzi wa shule zilizofaidika na msaada huo kuacha tabia
mbaya ya kuuza vitabu na kuwataka walimu wa shule hizo kufatilia kwa
makini wanafunzi wote watakaopatiwa vitabu hivyo.
Naye
Mwalimu mkuu wa sekondari ya Irole Laurence Maluka akiongea kwa niaba ya
wakuu wa sekondari 22 zilizofaidika na msaada huo wa vitabu alisema
msaada huo wa vitabu utaweza kuwa saidia wanafunzi kuwa na uweza wa
kujisomea zaidi na kuwawezesha kufaulu hadi kwenda chuo kikuu,kwani hapo
awali kulikuwa na changamoto kubwa katika shule zetu ambapo uwiano
ulikuwa kitabu kimoja wanafunzi 5 lakini kwa sasa ni vitabu 5 kwa
mwanafunzi mmoja.
“Ni
jambo la kulishukuru sana shirika la CAMFED kwa msaada huu utapunguza
zaidi, kwa kweli huu ni msaada mkubwa katika kuboresha taaluma na kuinua
ufaulu hivyo tunaomba program hii ya shule zetu iendelee ili kuwafikiwa
wanafunzi wengi zaidi katika wilaya ya Kilolo” alisema Maluka
Kwa
upande wake Afisa Miradi wa CAMFED Tanzania, Christina Kyaruzi amewataka
wanafunzi wa sekondari zote wilaya ya Kilolo mkoani Iringa kuongeza
uwezo wa kujisomea ufaulu wa wanafunzi unaongezeka kupitia msaada
unatolewa na shirika hilo.
Alisema vitabu
hivi vitunzwe ili viweze kuwafaidisha wanafunzi wengi kwa
kuwa vitaleta faida kwa wanafunzi wengi zaidi katika kujisomea na
kuwataka walimu wakuu wawapatie wanafunzi kila mmoja vitabu vitano na
kwenda navyo nyumbani hadi amalizapo elimu ya sekodari na kuweza
kuvirudisha.
Alizitaja
shule zilizofaidika na msaada huo ni shule ya sekondari Ilula,
Nyalumbu, Mazombe, Irole,Lundamatwe, Selebu, Ngangwe, Uhambingeto,
Lukosi, Mlafi Na Ndekwa.
Shule
nyingine ni shule za za sekondari za Mtitu, Kilolo, Lulanzi,Ukwega,
Udzungwa, Dabaga, Kitowo, Mawambala, Masisiwe, Madege na Makwema.
Post a Comment