Mwenyekiti
wa kamati ya mashinda ya Tunzo ya Ushairi nchini Tanzania Ibrahim
Seushi akizungumza wana wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa
uzinduzi wa Tuzo hizo mapema hivi karibuni. Tuzo hizo zitaitwa Ebrahim
Hussein ikiwa ni kumuenzi nguri na mkongwe huyo wa mashairi hapa nchini.
Profesa
Ebrahim Hussein (katika) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa
uzinduzi wa tuzo za mashairi zilizopewa jina lake ikiwa ni kuenzi
mchango wake katika tasnia hiyo mapema hivi karibuni.
Mkurugenzi
wa Mkuki na Nyota Publisher Bw. Walter Bgoya akifafanua jambo wakati wa
uzinduzi wa tuzo za mtunzi wa mashairi ambapo kampuni hiyo ndiyo
muendeshajio wa mashindano hayo.
Jaji
Kiongozi wa Tuzo za Ebrahim Hussein Profesa Mugabyo Mlinzi Mulokozi
akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa tuzo hizo mapema hivi karibuni.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Bi. Hajaty Shani Kitoga akiimba shairi la Wakati
Ukuta ambaole ni moja ya kazi za Profesa Ebrahim Hussein wakati wa
uzinduzi wa tuzo za mashairi zilizoanzishwa mapema hivi karibuni.
Profesa
Ebrahim Hussein (katika) akiwa katika picha ya pamoja na wageni
waalikwa wakati wa uzinduzi wa tuzo za mashairi zilizopewa jina lake
ikiwa ni kuenzi mchango wake katika tasnia hiyo mapema hivi karibuni.Picha zote na Frank Shija – WHVUM
Post a Comment