Kilimanjaro
Tanzania Music Awards (KTMA2014),
ni tuzo ambazo hufanyika kila mwaka kwa lengo la kutambua kazi bora za
wasanii ambazo zimefanya vizuri ndani ya mwaka mzima. Mapema hii leo,
Meneja wa bia ya Kilimanjaro, Bwana George Kavishe alifungua tuzo hizo
rasmi na kutoa maelezo kwa mabadiliko ambayo yamejitokeza mwaka huu…
Baadhi ya mabadiliko ambayo yataonekana safari hii, ni kwa mara ya
kwanza mashabiki watakuwa na nafasi ya kupendekeza kwa njia ya SMS,
barua pepe na kupitia tovuti jina la msanii, kikundi au mtayarishaji wa
Muziki aliefanya vizuri.
Kampuni ya
bia ya Tanzania (TBL) kwa ushirikiano na Baraza la Sanaa Tanzania
(BASATA) leo tumezindua rasmi msimu mwingine wa Tuzo za Muziki Tanzania
zinazojulikana kama KTMA.
Mkutano na
wana habari za michezo na burudani kutoka vyombo mbali mbali ndio
umezindua msimu huu katika hoteli ya Kebby’s ilioko maeneo ya Mwenge
jijini Dar es Salaam. Viongozi wa BASATA pamoja na wa bia ya
Kilimanjaro walizungumzia mabadiliko chanya katika mchakato wa mwaka huu
ikiwa ni
juhudi na hatua za kuendelea kuboresha mfumo wa upatikanaji wa wateule wa vipengele mbali mbali vya tuzo hizi.
Mabadiliko:
Mwaka huu
watanzania wamepewa fursa ya kupendekeza wasanii, nyimbo, vikundi,
watayarishaji, video n.k wanazodhani zinastahili kuwepo kwenye mchakato
wa kuwapata wateule wa tuzo za muziki Tanzania. Kwakutumia mfumo wa
SMS na mtandao wapenzi wa muziki wataweza kutoa mapendekezo yao
kupitia;
a. Namba ya simu 15440.
b. Mtandao – Website/tovuti na barua pepe/email.
Semina fupi ilioendeshwa katika hoteli ya Kebbys ilitoa ufafanuzi wa jinsi ya
kutoa mapendekezo na wapi mpenzi wa muziki anaweza kwenda kupata
maelezo ya ziada yanayohusiana na njia za kutumia kupendekeza kazi na
wasanii wanaowataka.
“Baada ya
tathmini ya mwaka jana, tumeonelea wakati wa kuwahusisha wapenzi wa
muziki umewadia. Tuzo za muziki ni mchakato endelevu unaoendelea
kubadilika kila mwaka ikiwa ni jitihada za kuboresha na kuhakikisha
mfumo unakua imara, kuhakikisha tunapata wateule na washindi
wanaostahili’. Alisema George Kavishe meneja wa bia ya Kilimanjaro.
‘Kama una amini msanii unaempenda ama kikundi ama wimbo n.k inastahili kuingizwa kwenye mchakato, basi pendekeza.’ Alisema George.
BASATA waliwapongeza
TBL kwa kuendelea kuwa wabunifu na kuwa makini na tathmini pamoja na
taarifa mrejesho (feedback) za wapenzi wa muziki na kuendelea kuzifanyia kazi alimradi kuboresha mfumo mzima wa tuzo hizi za kitaifa.
“BASATA ilipewa
nafasi ya kutathmini mchakato huu mpya na tumeuridhia na kuonelea ni
mfumo mzuri wenye tija na utakaoleta matoke mazuri zaidi kwa mchakato wa
tuzo hizi.” Alisema mwakilishi wa BASATA.
Taarifa kamili za njia ya kupendekeza zipo kwenye mtandao wa Kili http://www.kilitime.co.tz/ktma pamoja na page ya facebook ya Kilimanjaro na kwa taarifa unaweza kuifata handle ya kili @kilimanjarolarger kwenye twitter.
Usiku wa tuzo unatazamiwa kuwa ni tarehe 3-Mei-2014 katika ukumbi wa Mlimani City.
Kwa taarifa
zaidi wasiliana na wasimamizi wa taarifa na mchakato wa KTMA, 1Plus
kupitia anuani ilioainishwa hapo chini au na George Kavishe,
meneja wa Kilimanjaro.
Post a Comment