Afisa
Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia
Nkhoma Ledama, akibadilishana mawazo na Mwalimu Mkuu wa Shule ya
Sekondari Kikuyu Mwl. Zaituni Mkoyi alipotembelea shuleni hapo kwa lengo
la kuwahamasisha wanafunzi kuanzisha vilabu vya Umoja wa Mataifa.
Katikati ni Mwalimu Mkuu msaidizi wa shule hiyo Bw. Francis Tumaini.
Afisa
Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia
Nkhoma Ledama, akisaini kitabu cha wageni cha shule ya Sekondari Kikuyu
iliyopo mkoani Dodoma.
Afisa
habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia
Nkhoma Ledama, akizungumza na vijana wa shule za sekondari Kikuyu
iliyopo mkoani Dodoma, kuwaelezea umuhimu wa kujiunga na vilabu vya
Umoja wa Mataifa (UN Clubs) vinavyoanzishwa mashuleni kwa lengo la
kuwasaidia kujitambua na nafasi yao kama vijana katika kutekeleza agenda
mbalimbali za Umoja wa Mataifa.
Bi.
Ledama amefafanua kuwa, kuanzisha vilabu hivyo shuleni hapo
kutawawezesha kujifunza shughuli za Umoja wa Mataifa duniani,
kuhusishwa na mashirika mengine ya kimataifa, kushiriki katika mafunzo
mbalimbali, warsha na mikutano ndani na nje ya nchi kama vile National
Model UN, the Eastern Africa Model UN, the Africa Regional Model UN na
mengineyo, ikiwemo kupata nafasi ya kuisaidia jamii zao kupitia program
mbalimbali ikiwemo na masuala ya Kidiplomasia.
Bi.
Usia pia amewafafanulia vijana hao kuwa katika klabu hizo wataweza kuwa
na mtandao na vijana wengine kitaifa na kimataifa, kupata nafasi ya
kufanya kazi za kujitolea.
Pia
amewagusia suala la kujiepusha na marafiki wenye tabia mbaya
itakayowapelekea kujihusisha na vitendo visivyo vya kimaadili ikiwemo
uvutaji bangi na matumizi ya madawa ya kulevya, ambayo ni moja ya
changamoto kubwa inayoikabili Tanzania kwa sasa, aidha amewasaa
kutojihusisha na ngono pindi wawapo mashuleni ili kujiepusha na gonjwa
hatari la Ukimwi. (Pichani kushoto ni Mwalimu Cecilia Mwolo na Mwalimu
Elias Ndangula na Kulia ni Bw. Laurean Kiiza kutoka UNIC Dar es Salaam).
Mmoja wa wanafunzi shule ya Sekondari Kikuyu akiuliza swali kwa Afisa Habari wa Kitengo cha Habari (UNIC) hayupo pichani.
Sehemu ya Wanafunzi vidato mbalimbali wa shule ya Sekondari Kikuyu wakimsikiliza Bi. Usia Nkhoma Ledama.
Post a Comment