Ndugu zangu waandishi wa habari
Habari za kazi, na hongereni sana kwa kazi nzuri ya habari mnayoifanya katika jamii yetu.
Ndugu
zangu nimewaiteni hapa ili kusema machache na kuendelea kutoa maoni
yangu binafsi kama mwanachama hai wa Umoja wa vijana (Uvccm) kuhusu
kumsisitiza mzee John Samwel Malecela auombe radhi Umoja wa vijana
waTanzania kwa kitendo chake cha kuunga mkono tamko lilitolewa na mkuu
wa idara ya uhamasishaji na chipukizi wa uvccm Tanzania Ndg Paul Makonda
Msisitizo
wangu unatokana na jinsi gani nilivyosikitishwa na kitendo
alichokifanya Mzee Malekela cha kumuunga mkono ndg Makonda,, ambae tamko
lake limekataliwa na Mwenyekiti wetu wa Taifa ndg Sadifa Juma Khamis,
kwamba si la umoja wa vijana na si vema kwa wanachama kusemana nje ya
vikao, pia makamu mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Tanzania Ndg Mboni
Muhita pia amelikataa ya kwamba halitokani na Umoja wa vijana, ikumbukwe
kwamba Makamu Mwenyekiti ni mtu wa pili kiitifaki katika umoja wa
vijana ukilinganisha na Ndg makonda ambae ni watano katika uvccm. Na ni
kiongozi wa idara tu. Mzee malekela kuliunga tamko la Makonda ni kinyume
cha utaratibu na amewakosea heshima viongoz wetu wa vijana wa taifa na
uvccm yote kwa ujumla.
Mbali na
hilo, pia tamko la ndg Makonda limebeba misamiati tata ambayo
imesababisha mgongano wa hoja baina ya viongoz wa kiimani na waumini wao
wa madhehebu yote ambayo pia ni sehemu ya taifa hili.. mgongano huo wa
viongoz wa kiimani na Chama unaweza ukakiathiri Chama chetu kwa kiasi
kikubwa.
Ni rahisi
sana kwa viongozi wa kiimani kumsamehe ndg Makonda kutoka na rika lake,
lakini ni vigumu sana kumuelewa Mzee wa chama kwa kuunga mkono na
wanaweza wakahisi kwamba chama kimemtuma ndg Makonda kwenda kuwahusisha
katika tamko lake, jambo ambalo sio la kweli. Lkn pia nasikitishwa sana
kumuona Mzee wetu huyu kuunga mkono tamko linalomdhalilisha mkt wetu wa
vijana taifa na watendaji wake kwa mtu mmoja kuivunja kanuni mbele yao,
huku akiudanganya umma kwamba ni tamko la Uvccm..
Ndugu zangu waandishi, naendelea kusisitiza kwamba Mzee Malecela auombe radhi umoja wa vijana Tanzania..
Pamoja na
hayo,, pia napenda kutoa maoni yangu binafsi kuhusu maelezo ya mkt wa
uvccm mkoa wa Morogoro aliyoyatoa jana kwa waandishi wa habari, yale
yalikuwa ni mawazo yake binafsi na sio ya umoja wa vijana kwakuwa
hayajapitia katika kikao cha kamati ya utekelezaji cha mkoa,, amefanya
vema kuujulisha umma kwamba maoni niliyoyatoa mimi awali yalikuwa ni
maoni yangu binafsi na si ya uvccm mkoa kama nayeye pia maoni aliyoyatoa
ni yake binafsi na si ya uvccm mkoa waMorogoro. Na chama kinaruhusu
mtu kutoa maoni yake binafsi, nampongeza sana
Lakini
pia, si jambo jema kwa kila anayetoa maoni binafsi kuhusu mustakabali wa
chama, kuyahusisha maoni yake na maswala ya makundi,, na chama chetu
hakijamzuia mwanachama yeyote mmoja mmoja kutoa maoni yake binafsi,,
tukianza kuwanyima fursa wanachama kutoa maoni yao kwa mihemko ya
makundi, basi tutaikandamiza demokrasia ya ndani ya chama, kama viongoz
ni lazima tujue kutofautisha kati ya vichwa vya habari vya habari na
habari yenyewe, vinginevyo kutokana na ukubwa wa chama na maoni
yanayotolewa na wanachama wa maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi,
kutakuwa na watu wa kukanusha au kurekebisha, na wale wa kutoa maoni,
CCM ni chama cha wanachama wote,, pasiwepo namna yeyote ile ya kunyimana
uhuru.
Nungana
na Mwenyekiti wa uvccm mkoa wa Morogoro kumpongeza sana mkt wetu mpendwa
na rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania mhe Jakaya Mrisho Kikwete
kwa hotuba yake nzuri aliyoitoa mkoani Mbea hivi karibuni katika sherehe
za kutimiza miaka 37 ya chama chetu imara cha CCM, ni wajibu wetu sote
kuyatekeleza yale aliyotuagiza mhe mkt wetu wa CCM taifa. Na hasa
kuheshimu maamuzi yatokanayo na vikao
Ndg zangu
mkoa wa Morogoro umekumbwa na matatizo mengi sana, ikiwa pamoja na
mapigano ya wakulima na wafugaji, na mafuriko yaliyotokea wilayani
kilosa na mvomero,, nami napenda kutoa pole kwa wahanga wa matatizo
hayo, na kuunga mkono maoni ya mkt wa uvccm mkoa kwa wadau mabalimbali
kujitokeza katika kusaidia wahanga, pia nawapongeza sana viongozi wa
serikali na chama wote kwa kuwajibika kutatua na kusaidia katika swala
hili..
akini ni
vema sana kwa sisi vijana kuwa wa kwanza na mstari wa mbele kufika
katika maeneo ya matukio mapema ili kuona hali na kushiriki katika hatua
za awali,, tusijifunze kutoa pole kwenye vyombo vya habari baada ya
matukio kuwa yameshapita na hatujafika hata eneo lenyewe la tukio.. hapo
tutakuwa tunaonekana tunafanya siasa badala ya kazi.. lakini kutoa
maelekezo au wito katika maeneo ya majanga ambayo tayari mkt wetu wa
taifa ameshafika na kufanya hivyo, ni makosa ambayo tunahitajika
kujifunza…
Napenda
sana kutoa pongez zangu binafsi kwa vijana wa uvccm wilaya ya mjini na
wale wa kilosa kwa jinsi wanavyoshiriki kikamilifu katika shughuli za
kampeni katika katika chaguz za marudio kata ya tungi na ludewa, ni
maoni yangu binafsi kwamba na sisi wanachama wengine tushiriki
kikamilifu, badala ya kutoa maoni huku tukiwa hatujawahi hata kufika
katika eneo la tukio. Hasa katika maeneo amabayo kuna chaguzi za marudio
ndani ya taifa letu
Pia ni
maoni yangu kwa vyama siasa hususani chadema kuacha kampeni za vurugu na
kujeruhiana ambazo zinawadhuru wananchi, kuwanyima amani na kuzorotesha
shughuli zao za kiuchumi, tufanye kempeni za kiistarabu, za hoja na
amani kama ilivyo desturi ya nchi yetu, pia vyombo vya ulinzi naviomba
viongeze umakini zadi katika kipindi hiki hasa katika maeneo yale ambayo
kampeni zinafanyika..
Asanteni kwa kunisikiliza, nawatakia kazi njema!!
IMETOLEWA NA
HERI HOZA
Mjumbe wa kamati yautekelezaji ya baraza la UVCCM
Mkoa wa Morogoro



Post a Comment