Na Andrew Chale
WABUNIFU mbali
mbali watakaopamba miaka 10 ya onyesho la mavazi lijulikanalo kama
‘Lady in red Super brand, 10th Anniversary’ linalotarajiwa kufanyika
Februari 14, tayari majina yao yamewekwa hadharani. Onyesho la mwaka huu linatarajia kufanyika kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam, Februari
14, huku asilimia ya mapato ya fedha hizo zinatarajia
kusaidia wathirika wa dawa za kulevya wa kituo cha Kikale Kilichopo
Mkoani Pwani.
Akiongea na wandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Fabak Fashions inayoandaa onyesho hilo, Asia Idarous Khamsin, alisema kila mwaka onyesho hilo huja kitofauti ikiwemo kuongeza vionjo mbalimbali katika kufikia mafanikio kwenye tasnia ya ubunifu na mitindo ya mavazi hapa nchini.
“Safari hii, steji ya Lady in red’, inatimiza miaka 10, huku ikijivunia kuibua
vipaji vya wabunifu wengi hapa nchini, na wengine kwa sasa wanamajina
makubwa kwenye yasnia hiyo, hivyo tutaendelea kutoa nafasi kwa wabunifu
chipukizi mara kwa mara ilikufikia malengo yao” alisema Asia Idarous.
Asia Idarous aliwataja wabunifu magwiji watakaopamba steji hiyo kuwa ni
pamoja na Khadija Mwanamboka, Mustapher Hasanal , Ally Remtulla, Lucky
Creation, Martin Kadinda, Ghymkana Hilali, Paka wear, Gabriel Molel,
Fransiska Frankoo, Shirima, Salim Ally, Ameed Abdul, Mgese Makory, Kiki
Collection, Rose fashion, Diana Magesa, Rio Paul na wengine.
pamoja na Khadija Mwanamboka, Mustapher Hasanal , Ally Remtulla, Lucky
Creation, Martin Kadinda, Ghymkana Hilali, Paka wear, Gabriel Molel,
Fransiska Frankoo, Shirima, Salim Ally, Ameed Abdul, Mgese Makory, Kiki
Collection, Rose fashion, Diana Magesa, Rio Paul na wengine.
Kwa upande
wa wabunifu chipukizi watakaopamba ni pamoja na Faustin Simon, Water
Edward, Brian Hango, Benedict Mnzava,Crissiwelly Uissoson,Willex
Willibard, Jackson, Gumbala, Jabir Jumanne, Alabama King, Agusta
Masaki, Nelson Tomas, Bebi Juliet Mtandu, Ummi fashion/Ummi Investiment
Company, Asmahan Eva, Hassan Nasor, Juniper Mafuru, Ante Ngongi, Adam
Hassan, Jaquline, Kijangwa na Waiz Shelukindo.
Aidha, Asia Idarous aliongeza kuwa, kwenye onyesho hilo,
pia kutakuwa na burudani mbalimbali ikiwemo kutoka bendi ya Babloom
Trio na Mwanamuziki mahiri wa nyimbo na ngoma za asili, Wanne Star.
Katika onyesho hilo ambalo litafanyika siku hiyo ya
Februari 14, ambayo pia itakuwa ni siku ya Wapendanao ‘Valentine’s Day’ ,
kiingilio kitakuwa sh 30,000 kwa viti vya kawaida huku viti maalum
ikiwa sh 50,000. Tayari tiketi za onyesho hilo zimeanza
kuuzwa ikiwemo vituo vya duka la Fabak fashion, lililopo mikocheni
mkabala na kituo cha Mwalimu Nyerere huku kwenye hoteli ya Serena,
zikipatikana mapokezi.
mkabala na kituo cha Mwalimu Nyerere huku kwenye hoteli ya Serena,
zikipatikana mapokezi.
Kwa upande wa wadhamini wakuu wa shindano hilo ni
pamoja na kinywaji cha Zanzi pamoja na kampuni ya nywele ya Darling.
Wengine ni CXC, Times fm, Clouds media, Vijimambo blog, michuzi media
group, channel ten, Elite Computer, Eventlites, One touch-solution,
Raysa Style, Paka Wear, Dj Bula, Magic fm, DTV, Jambo Leo, I View media,
Vayle Spring, Voice of American na wengine wengi.
Post a Comment