Wachezaji
31 wameteuliwa kujiunga na timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya
miaka 20 (Ngorongoro Heroes) kwa ajili ya michuano ya Afrika ambayo
fainali zake zitafanyika mwakani nchini Senegal.
Ngorongoro
Heroes itakayokuwa chini ya Kaimu Kocha John Simkoko akisaidiwa na
Mohamed Ayoub inaingia kambini kesho (Machi 19 mwaka huu) jijini Dar es
Salaam kujiandaa kwa mechi ya kwanza dhidi ya Kenya itakayochezwa kati
ya Aprili 4-6 jijini Nairobi.
Kikosi
kinachounda timu hiyo ambayo itarudiana na Kenya kati ya Aprili 25-27
mwaka huu jijini Dar es Salaam kinajumuisha pia baadhi ya wachezaji
walioonekana katika mpango wa ung’amuzi wa vipaji kwa ajili ya maboresho
ya Taifa Stars.
Wachezaji
walioitwa ni makipa Aishi Manula (Azam), Hamad Juma Hamad (Scouting-
Temeke), Manyika Peter Manyika (Scouting- Ilala) na Mwinyi Hassan Hamisi
(Mtende, Zanzibar).
Mabeki
wa pembeni ni Ayoub Semtawa (Coastal Union), Edward Charles (JKT Ruvu),
Frank Linus Makungu (Scouting- Rukwa), Gabriel Gadiel Michael (Azam),
Hussein Mkongo (Ashanti United) na Ibrahim Said Mohamed (Chuoni,
Zanzibar). Mabeki wa kati ni Bashiru Ismail (Tanzania Prisons), Faki
Rashid Hakika (Ashanti United) na Pato Ngonyani (Majimaji).
Viungo
ni Ally Nassoro (Coastal Union), Bryson Raphael (Azam), Farid Musa
(Azam), Hamid Mohamed (Mbeya City), Hassan Mbande (Mtibwa Sugar),
Ibrahim Mohamed Ibrahim (Scouting- Ilala), Idd Seleman (Ashanti United),
Mohamed Issa Juma (Acudu, Afrika Kusini), Muhsin Ally Muhsin (Scouting-
Kinondoni), Seleman Magoma (Scouting- Ruvuma) na Tumaini John
(Scouting- Mwanza).
Washambuliaji
ni Ally Salum Kabunda (Ashanti United), Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto,
Zanzibar), Jafari Mwambusi (Mbeya City), Kelvin Friday (Azam), Ramadhan
Bilal (Mlale JKT), Salum Abdilah Mineli (Ndanda) na Sibiank Lambard
(Tanzania Prisons).
Post a Comment