MWENYEKITI
wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, jana ametangaza rasmi kwamba
hatagombea tena nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo
unaotarajiwa kufanyika Mei 4 mwaka huu.
Hata
hivyo Rage kabla ya kutangaza maamuzi yake ya kutotetea cheo hicho
katika uchaguzi mkuu ujao, wanachama wa klabu hiyo walianzisha vurugu
katika mkutano mkuu huo uliotishwa maalumu kwa ajili ya kufanya
marekebisho wa katiba kutokana na kiongozi wao huyo kuwaita ‘mbumbumbu’.
Kufuatia
kauli hiyo, Rage, alilazimika kuwaomba radhi wanachama hao zaidi ya 571
waliohudhuria mkutano huyo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Bwalo la
Polisi, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
“Napenda
kuwaomba radhi wanachama wenzangu kutokana na nilivyosema tuache
umbumbumbu, lakini sikuwa namaanisha kama wengi wenu mlivyoelewa,”
alisema Rage.
Licha
ya kusema hatagombea tena uongozi, Rage, alisema ataendelea kuwa
mwanachama mwaminifu wa Simba na atatoa mchango wake ili kufanikisha
maendeleo.
“Nitatoa mchango wangu wa hali na mali, sina ugomvi na mtu yoyote na bado nina mapenzi na Simba,” aliongeza.
kusoma zaidi bofya hapa chini
Post a Comment