Daktari
Bingwa wa Ubongo, Mgongo na mishipa ya fahamu Dr. Othman W. Kiloloma
kutoka hospitali ya Muhimbili amesema kuwa timu ya madaktari saba
imewasili kutoka Muhimbili ikiwa na daktari bingwa 1 wa usingizi wakiwa
na vifaa vyote muhimu ili kuungana na madaktari Bingwa wa upasuaji
Bugando kwaajili ya kuweka kambi ya tiba mkoani Mwanza.
|
Dr.
Othman W. Kiloloma ameongeza kuwa dhana ya kuweka kambi Mwanza imekuja
ikiwa ni hatua ya kujaribu kupunguza vifo na usumbufu unaowakumba watu
wenye maradhi hayo pindi wanapohitaji tiba ambapo wengi wameshindwa
kupata huduma mapema kutokana na kushindwa kuzimudu gharama kwa magonjwa
hayo ambayo kila kukicha idadi ya watu wenye matatizo ya Ubongo na
Mishipa ya fahamu inaongezeka. Ameishukuru sana African Barrick Gold kwa
kudhamini mpango huo.
|
Kama
upasuaji utahitaji kufanyika masaa 24 tuko tayari kwa hilo, nia ni
kuwahudumia wale wote watakao jiandikisha kuwa wanamatatizo na
wanahitaji tiba.
|
Mgeni
rasmi wa Uzinduzi wa mpango huo wa tiba, Mstahiki Meya wa jiji la
Mwanza ambaye pia ni diwani wa Kata ya Mkolani Mhe. Stanslaus Mabula
amewataka wananchi wote wenye matatizo kujitokeza kwani ni nadra sana
kupata tiba kama hiyo bure bila malipo, naye akisema kuwa ni mmoja
katiya waathirika wa matatizo hayo ambapo ni hivi karibuni tu! naye
ametoka kufanyiwa upasuaji wa matatizo ya mgongo katika Hospitali ya
Rufaa ya Taifa ya Muhimbili. Pia amewashukuru sana Madaktari hao bingwa
kwa kuliona tatizo na kulitafutia ufumbuzi sambamba na kuwashukuru
Kampuni ya ABG waliodhamini mpango huo.
|
Sehemu ya madaktari Bingwa watakao husika na zoezi hilo la tiba itakayo tolewa katika Hospitali ya Rufaa Bugando.
|
"Mpaka
sasa tumeandaa wagonjwa 33, ambao wanahitaji oparesheni, leo kuna
wagonjwa 12 ambao wamepangiwa oparesheni, watoto ni wa8 na watu wazima
ni wa4". Miongoni mwao kuna wagonjwa wenye matatizo makubwa wawili,
mmoja anausaa kwenye ubongo, mwingine damu imeingia kichwani" alisema
Dr. Gerlard ambaye ni Bingwa wa upasuaji kutoka Hospitali ya Rufaa
Bugando (BMC ambao ni wenyeji).
|
Kutoka
kushoto ni Mkurugenzi wa Bugando (BMC) Prof. Charles Majinge, Meneja
Mahusiano na jamii wa Kampuni ya ABG Steve Kisake, mgeni rasmi Mstahiki
Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula na kulia ni mmoja kati ya
madaktari bingwa wakisikiliza maelezo na ufafanuzi wa jinsi zoezi
litakavyo fanyika.
|
Ni mmoja kati ya akinamama waliojitokeza kwa kuwaleta watoto wao kufanyiwa upasuaji wa mishipa na mgongo.
|
Ni
uvimbe wa mmoja kati ya watoto wanao subiri tiba. Kila la kheri
Mwenyezi Mungu awaongoze na mfanikishe kwa wale wote wanaopata tiba na
wale wanao subiri tiba.
|
Ni
mtoto ambaye anasubiri kupatiwa tiba kwa tatizo la kichwa kujaa maji
kwa tiba ya bure itakayo tolewa na madaktari bingwa wa upasuaji toka MOI
na BMC akiwa katika ward ya Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza.
Kila la kheri Mwenyezi Mungu awaongoze na mfanikishe kwa wale wote
wanaopata tiba na wale wanao subiri tiba.
|
Tatizo la kichwa.
|
Tatizo la uvimbe kwenye mgongo.
|
Baadhi
ya akinamama wakiwa na watoto wao katika ward wakisubiri kupatiwa tiba
kwa matatizo mbalimbali yanayo hitaji upasuaji unaofanywa na madaktari
bingwa wa upasuaji toka MOI wakishirikiana na mabigwa wa upasuaji wa
BMC, ni katika Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza.
|
Dr.
Othman W. Kiloloma akitoa ufafanuzi katika kusanyiko la uzinduzi wa
tiba ya bure kwa maradhi ya Kichwa, Mgongo na Mishipa uliofanyika ukumbi
wa mikutano kitengo cha Satatani Bugando jijini Mwanza.
|
HALI IKIWA TETE KANDA YA ZIWA NAKO WODI ZA MOI ZIMEFURIKA.
MWANZA.
LICHA ya
kuwa na Madaktari bingwa wa upasuaji wa kichwa wasiozidi watano tu
nchini, wodi za kitengo cha upasuaji wa kichwa na mifupa cha Hospitali
ya Rufaa ya Taifa Mhimbili (MOI) jijini Dar es Salaam, zimefurika
wagonjwa.
Mratibu
wa jopo la madakatari bingwa saba wa MOI walioweka kambi maalum ya
matibabu ya mgongo na upasuaji kichwa katika Hospitali ya Rufaa ya
Bugando (BMC) jijini Mwanza, Dkt Othman Kiloloma, amesema hali hiyo ni
moja ya changamoto kubwa inayokikabili kitengo hicho.
Amedai,
kutokana na kusubiri matibabu hayo kwa muda mrefu, baadhi ya wagonjwa wa
nje ya Dar es salaam huishiwa fedha za kujikimu na hata nauli, hivyo
Madkatari hao kulazimika kuwasaidiwa nauli za kuwarudisha makwao.
Dkt
Kiloloma alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari
muda mfupi kabla ya uzinduzi wa Matibabu ya mgongo na upasuaji kichwa
unaofanywa na wataalam hao hapa, kwa kushirikiana na madakatari bingwa
wa BMC.
Matibabu
hayo yanayotolewa bure kwa ufadhili wa kampuni ya African Barrick Gold
katika hospitali ya Bugando, yalianza juzi (Machi 24) na yataendelea
hadi Machi 28 mwaka huu ambapo wagonjwa zaidi 33 wanatarajiwa kufanyiwa
upasuaji mkubwa wa vichwa na kutibiwa migongo.
“Wodi
zetu zimejaa wagonjwa wetu wanasubiri kwa muda mrefu, ukituletea mgonjwa
atalala wapi wakati wamejaa hadi kwenye makorido lakini hatuwezi
kuwafukuza.” Alieleza Dkt Kiloloma wakati akionyesha picha za wagonjwa
waliolazwa MOI, walivyofurika.
Alisema
kupeleka wagonjwa wa aina hiyo Dar ni gharama kubwa hivyo ndiyo maana
jopo hilo kwa ufadhili wa kampuni hiyo ya uchimbaji madini nchini,
limeweka kambi Bugando ili kuwasaidia wagonjwa waliopo kanda ya ziwa
ambao ingebidi wapelekwe Mhimbili au nje ya nchi kwa matibabu hayo.
“Kati ya
Madaktari saba tuliotoka MOI kuja Mwanza kuungana na wenetu wa Bugando
kusaidia wangonjwa wa Kanda hii ya ziwa, mabingwa wa upasuaji wa kichwa
tupo watatu. Tanzania nzima ina mabingwa wa Upasuaji kichwa wasiozidi
watano, hivyo wawili ndio wamebaki Dar.” Alieleza bingwa huyo na kudai
upungufu wa wataalamu hao ni changamoto kubwa inayolikabili taifa.
Alieleza
kwamba kukamilika kwa jengo la ghorofa nane linalojengwa MOI kutasaidia
kuondoa mlundikano wa wagonjwa ambao sasa wanakosa pa kulala licha ya
wengine kuwa nje ya wodi wakisubiri matibabu.
“Tunapasua
wagonjwa 600 kwa mwezi lakini kutokana na kusubiri matibabu kwa muda
mrefu kidogo, baadhi au wauguzi wao huishiwa fedha za kujikimu na
kulazimika kuwasaidia nauli ya kurudi kwao, wengine (akina mama) hukuta
waume zao walisha oa wanawake wengine.” Alidai.
Post a Comment