|
Mkurugenzi
Msaidizi wa Biashara Juma Boma ambaye amesema kwa kuanzia shirika lake
litafanya safari nne kwa juma kwa gharama ya shilingi laki moja na elfu
hamsini tu kwa safari moja ya kwenda. |
|
Marubani wa Ndege hiyo |
|
Patrick
Itula ambaye ni Mkurugenzi msaidizi wa Ufundi wa shirika hilo amesema
hivi sasa Mkoa wa Mbeya unazo fursa za kukuza biashara kupitia shirika
lake kutokana kuwa na mpango wa kuunganisha safari zake kutoka Mbeya na
kwenda mikoa ya kaskazini na kanada ya ziwa.
|
|
Rubani
wa ndege hiyo Richard Shaidi ameipongeza serikali kwa kukamilisha
uwanja huo kwani ni mzuri na umekuwa miongoni mwa viwanja bora nchini na
unaweza kutua wakati wowote kutokana na kufungwa vifaa vya kisasa. |
|
Shirika la
ndege nchini[ATC]limeanza safari za anga kutoka Dar es Salaam na Mbeya Machi 17
mwaka huu.
Safari ya
kwanza ya ndege hiyo imezinduliwa rasmi na Mkurugenzi Msaidizi wa Biashara Juma
Boma ambaye amesema kwa kuanzia shirika lake litafanya safari nne kwa juma kwa
gharama ya shilingi laki moja na elfu hamsini tu kwa safari moja ya kwenda.
wanazo ndege
bora ambazo wasafiri watafurahia huduma zake wawapo safarini, Boma amesema
shirika lake limejipanga vema kukabiliana na ushindani uliopo .
Pia amesema
kuwa shirika lake limezingatia matakwa ya wateja hivyo ndege zake zitaanza safari
Dar es Salaam saa sita mchana na kufika Mbeya saa saba mchana ili kuwawezesha
abiria wanaotoka nchi jirani kusini mwa Afrika kuwahi safari ili kutumia ndege
za ATC.
Aidha
Patrick Itula ambaye ni Mkurugenzi msaidizi wa Ufundi wa shirika hilo amesema hivi
sasa Mkoa wa Mbeya unazo fursa za kukuza biashara kupitia shirika lake kutokana
kuwa na mpango wa kuunganisha safari zake kutoka Mbeya na kwenda mikoa ya
kaskazini na kanada ya ziwa.
Itula
amesema kuwa pia wana mpango wa kuanzisha safari za kwenda Congo na Zambia
kupitia Mbeya ili kuimarisha zaidi biashara ya utalii kwani Mkoa wa Mbeya una
vivutio vingi hivyo Mkoa utatumia fursa kujitangaza.
Kwa upande
wake Rubani wa ndege hiyo Richard Shaidi ameipongeza serikali kwa kukamilisha
uwanja huo kwani ni mzuri na umekuwa miongoni mwa viwanja bora nchini na
unaweza kutua wakati wowote kutokana na kufungwa vifaa vya kisasa.
Na Mbeya yetu
|
on Thursday, March 20, 2014
Post a Comment